Mnenia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mnenia ni kata ya Wilaya ya Kondoa katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41709[1] .

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 13,056 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11528 [3] waishio humo.

Baadhi ya vijiji vya kata ya Mnenia vyenye shule ya msingi ni Mnenia yenyewe, Chungai, Filimo na Bambare. Asilimia kubwa za wakazi wa kata ya Mnenia ni Warangi.

Matamshi ya jina la Mnenia yameleta shida ya kuliandika kwa muda mrefu. Sababu yake kuwa matamshi siyo ni bali n ikifuatiwa na y, ila ny katika alfabeti ya Kiswahili ni sauti nyingine. Ndiyo sababu katika uandishi wa lugha ya Kirangi, jina la kata huandikwa Mʉnéen'ya. Kwa lugha ya Kiswahili wengine huandika Mnen'ya.

Kiuchumi Mnen'ya hujulikana hasa kama soko la vitunguu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. Sensa ya 2012, Dodoma - Kondoa DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
Kata za Wilaya ya Kondoa - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Bereko * Bumbuta * Busi * Changaa * Haubi * Hondomairo * Itaswi * Itololo * Kalamba * Keikei * Kikilo * Kikore * Kinyasi * Kisese * Kwadelo * Masange * Mnenia * Pahi * Salanka * Soera * Thawi


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mnenia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.