Mkude Simba
Mkude Simba | |
---|---|
Mkude Simba | |
Amezaliwa | Musa Yusuph Mahenge Desemba 30, 1986 Manzese, Dar es Salaam, Tanzania |
Jina lingine | Kitale, Teja, |
Kazi yake | Mwigizaji, mwigizaji wa sauti, mwimbaji |
Miaka ya kazi | 2002 |
Ndoa | Fatma Abbas |
Watoto | 2 |
Musa Yusuph Mahenge (amezaliwa Manzese, Dar es Salaam, 30 Disemba 1986) ni mwigizaji, mwongozaji na mwandishi wa filamu kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa uhusika wake wa Kitale ambao hucheza kama muathirika wa dawa za kulevya (teja) na Mkude Simba[1] kupitia vitangazo vidogo vya EFM Radio.
Mbali na uigizaji, Kitale ni mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva).
Mwaka wa 2010, alitoa wimbo unaoitwa Hili Dude Noma ambao alimshirikisha Corner na Midezoo, Mwaka (2012) alitoa wimbo mwingine unaoitwa Mbuzi Kagoma Kwenda,akimshirikisha Sharo Milionea na mkude, Nawaektia mwaka (2014) akimshirikisha Midezoo, Mithuni Chakraboty (2019).
Alianza kufahamika katika kundi la Kaole Sanaa Group kabla ya kuhamia rasmi Fukuto Arts Group la Tuesday Kihangala kati ya 2002/2003. Kwa Kihangala alifanya Rangi ya Chungwa (2003), Jumba la Dhahabu na Ua Jekundu.
Baadaye akatengeneza filamu zake mwenyewe ikiwa ni pamoja na Mbwembwe, Kubwa Jinga, Porojo, Bad Night na More Than a Lion.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Mkude alizaliwa na baba na mama wote Walugulu[2]. Alisoma katika shule ya msingi Manzese Uzuri, Dar es Salaam na kuhitimu 2001. Katika familia yao wapo sita, watano wamezaliwa baba na mama mmoja, Kitale wa kwanza - vilevile wa pili kwa upande wa baba kwa sababu alizaa mtoto wa kike kabla ya kumuoa mama yake na Kitale.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Kitale alianza kuigiza tangu akiwa Shule ya Msingi Uzuri. Alijiunga na Kaole Sanaa Group mnamo 2002. Kipindi angali anaishi Manzese, aliishi karibu na waigizaji maarufu wa kundi la Kaole, Abdallah Mkumbila (Muhogo Mchungu) na akina Swebe Santana. Nyakati hizo, alitamani sana kuigiza baada ya kuwaona walichokuwa wakikifanya. Alivyojiunga Kaole, alikutana na Tuesday Kihangala. Kupitia huyu, ilikuwa rahisi kufanya kazi Kaole. Tuesday na Mkude wanatoka kijiji kimoja huko Morogoro.
Kukatokea mfarakano baina ya Kihangala na kiongozi mkuu wa kundi la Kaole kipindi hicho Bwana Christian Muhenga na hatimaye Tuesday Kihangala akatoka na kuanzisha kundi lake la maigizo maarufu kama 'Fukuto Arts Group' akamchukua na Mkunde Simba. Akiwa huko, alishiriki katika tamthiilia ya Rangi ya Chungwa, Ua Jekundu na Jumba la Dhahabu kabla ya kwenda kufanya kazi za kujitegemea.
Filamu za kujitegemea
[hariri | hariri chanzo]Mkude alianza kuandika filamu zake mwenyewe mnamo mwaka wa 2009. Filamu ya kwanza ilikuwa Badnight. Zifuatazo ni filamu alizoandika na kuziongoza;
- Badnight - 2009.
- Mwembwe - 2009.
- More Than a Lion - 2010.
- Porojo - 2013.
- Chizi Kalogwa Tena - 2014.
- Harusi ya Teja - 2015.
- Stan Bakora - 2019.
- Mzee Ndigula - 2019.
- Kimbiji- 2019.
- Mkubwa Bure - 2019.
Mbali na filamu, Mkude pia alitoa tamthilia maarufu nchini Tanzania - Maneno ya Kuambiwa. Tamthilia inarushwa kupitia TV ya TVE naidhaa yake ya YouTube ya KitaleMkudeSimba.
Orodha ya filamu alichocheza
[hariri | hariri chanzo]- Chizi Kalogwa Tena.
- 4 Days Mission.
- Sina Jinsi.
- Mkweli Nani.
- Dini Imani.
- Msela.
- Utani.
- Zungusha.
- Bwege Mtozeni.
- Break Down.
- Shoe Shine.
- Street Girl.
- Chips Kuku.
- Zungu la Unga.
- Lakuchumpa.
- More than a Lion.
- Porojo.
- Mpela Mpela.
- Utanibeba.
- Jumba la Dhahabu Season 1.
- Vituko Show Vol. 10.
- Sons & Jobs.
- Mission Town.
- Simu ya Kichina.
- Alosto.
- Back from New York.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.youtube.com/watch?v=dCorrCZE3ns
- ↑ "Musa Kitale 'Kitale' | Actor, Commedian, Singer, — Bongo Movies - Buy Tanzania Movies and DVD's Online". www.bongocinema.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-09. Iliwekwa mnamo 2020-02-16.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkude Simba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |