Nenda kwa yaliyomo

Miriam Rodríguez Martínez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Miriam Elizabeth Rodríguez Martínez (5 Februari 1960 - 10 Mei 2017) alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu wa Mexico . Alikua mmoja wa "Wazazi Waliopoteza Watoto baada ya binti yake kutekwa nyara na kuuawa. Miriam aliuawa na watu wenye silaha waliovamia nyumba yake tarehe 10 Mei 2017.

Miriam Elizabeth Rodríguez Martínez alizaliwa tarehe 5 Februari 1960 huko San Fernando jimbo la Mexico la Tamaulipas . [1] Binti yake, Karen Alejandra Salinas Rodríguez, alitoweka mwaka wa 2012. [2] Mabaki ya Karen hatimaye yaligunduliwa mwaka 2014. [3] Rodríguez aliwafuata wauaji wa binti yake kwa miaka mingi. Baadhi ya wanaume waliokamatwa kwa kesi ya bintiye wametoroka gerezani baada ya kukamatwa. [2] Pamoja na kumtafuta binti yake, alikuwa akifanya jitihada za kuwasaidia wazazi wengine ambao watoto wao walikuwa wametoweka, na kutoka humo likaja tengenezo la Colectivo de Desaparecidos (The Vanished Collective).

Rodríguez aliuawa mnamo tarehe 10 Mei 2017, siku ambayo Mexico inaadhimisha Siku ya Akina Mama . Alipigwa risasi 12 na watu wenye silaha waliovamia nyumba yake, na kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitali. Kwa mshirikiano wake, waandamanaji walipaza sauti zao kupinga siku aliyouawa, wakitoa wito kwa serikali ya Mexico na Marekani kuhakikisha usalama wa watetezi wa haki za binadamu. [4]

  1. Juárez, Carlos Manuel (11 Mei 2020). "Tres años sin justicia en el asesinato de Miriam, la madre activista". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-20. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Villegas, Paulina (12 Mei 2017). "Gunmen Kill Mexican Activist for Parents of Missing Children". Iliwekwa mnamo 2020-03-08.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Obituary: Miriam Rodríguez Martínez died on May 10th". 20 Mei 2017. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Justice for Miriam Rodriguez" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 9 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Miriam Rodríguez Martínez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.