Nenda kwa yaliyomo

Milima ya Taurus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hii ni milima ya Taurus.

Milima ya Taurus (kwa Kituruki Toros Dağları) ni milima ya kusini mwa Uturuki inayotenganisha Bahari ya Mediteranea na mabonde ya Mesopotamia upande wa kusini na nyanda za juu za Anatolia upande wa kaskazini.

Safu za milima hii zina urefu wa kilomita 1,500 ikianza karibu na Ziwa Eğirdir kwenye magharibi na kuelekea hadi mpaka wa mashariki wa Uturuki.

Milima ya Taurus hugawanywa katika safu tatu kuu kutoka magharibi hadi mashariki kama ifuatavyo:

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Katika Taurus ya Kati (milima ya Aladaglar na Bolkar) mawe ya chokaa yamesababisha kutokea kwa maeneo ya karst ambako kiwango cha kawaida cha asidi katika mvua kilisababisha mmomonyoko ya miamba na kuunda baadhi ya mapango makubwa ya Asia.

Mto Manavgat huanzia mteremko wa kusini wa Beydaglari.

Katika historia safu za milima ya Taurus zilikuwa kizuizi kikubwa cha mawasiliano na usafiri kati ya Anatolia yenyewe na pwani ya bahari.

Mbali na kupanda mlima, kuna vituo viwili vya skii katika mlima, moja huko Davras karibu kilomita 25 (16 mi) kutoka miji miwili ya karibu ya Egirdir na Isparta, pili ni Saklıkent kilomita 40 (25 mi) kutoka mji wa Antalya.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Taurus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.