Michael Faraday

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Michael Faraday katika maabara yake
Uchoraji wa Michael Faraday

Michael Faraday (* 22 Septemba 179125 Agosti 1867) alikuwa mwanasayansi kutoka nchini Uingereza aliyegundua misingi muhimu kwa matumizi ya umeme. Utaalamu wake ulikuwa hasa upande wa fizikia na kemia.

Aligundua mdukizo sumakuumeme akaweka hivyo msingi kwa dainamo na mashine za kutengeneza umeme.

Upande wa kemia alifaulu kubadilisha gesi kadhaa kuwa kiowevu akagundua kanuni za elektrolisisi.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa kati ya watoto wanne wa familia maskini huko Newington Butts kusini ya London. Baba alikuwa mhunzi. Alisoma shule kwa miaka michache tu mengine akajifundisha mwenyewe. Alipofikia umri wa miaka 14 alipelekwa kama mwanafunzi kwa karahana ya kutengeneza vitabu na katika muda wa miaka saba alipata nafasi nyingi za kusoma vitabu alivyojalidi.

Baadaye alisikiliza masomo ya wanakemia mashujuri walioanza kumjua mwishowe aliajiriwa 1813 kama msaidizi wa maabara kwenye taasisi ya Royal Institution. Hapa alipanda ngazi kuwa msimamizi, mkurugenzi na hatimaye profesa wa kemia.