Miško Ražnatović
Miodrag "Miško" Ražnatović alizaliwa mnamo mwaka Septemba 16, 1966 ni mwanasheria na wakala wa michezo kutoka Serbia na alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu wa kulipwa. Yeye ni mwenyekiti, Afisa Mtendaji Mkuu, na mwanzilishi wa shirika la BeoBasket na wakala aliyethibitishwa na Fédération internationale de basket -ball.
Kama mmoja wa mawakala wanaoheshimika na wenye ushawishi mkubwa katika tasnia nzima ya mpira wa kikapu, Ražnatović alihusika katika majadiliano na kufanikisha mikataba mikubwa katika mpira wa kikapu barani Ulaya kote miaka ya 2000 na 2010.
kazi
[hariri | hariri chanzo]Ražnatović alicheza katika klabu nyingi kama vile, Napredak Kruševac, FMP, Radnički Belgrade, Ulcinj.
Taaluma ya Sheria
[hariri | hariri chanzo]Ražnatović alipata shahada yake ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Sheria cha Belgrade mnamo mwaka 1988. Miaka minne baadaye, alifungua kampuni yake ya sheria na kuanza kazi yake ya kisheria.
Pia, aliwakilisha mkurugenzi wa soka wa Serbia Radomir Antić katika mazungumzo yake ya mkataba na Shirikisho la Soka la Serbia (FSS) mnamo mwaka 2009.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Miško Ražnatović kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |