Mereba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mereba
Amezaliwa Marian Mereba
Septemba 19, 1990 (age 30)
Montgomery, Alabama
Kazi yake Mwimbaji • mtunzi wa nyimbo • mtayarashi wa muziki • mpiga gitaa • rapa
Miaka ya kazi 2013 hadi leo
Tovuti http://marianmereba.com/

Marian Mereba (anajita Mereba tu) ni Mmarekani na Mwethiopia mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, rapa, na mpiga gitaa.

Alianza kazi ya muziki jijini Atlanta, jimbo la Georgia, na sasa anaishi jijini Los Angeles.[1]

Kutoka albamu wa kwanza mpaka sasa, Mereba alifanya kazi na wanamuziki wengi, kama EARTHGANG, JID, 6LACK, Spillage Village wote, na wengineo[2], kiasi kwamba yeye aliwaita marafiki wake wa karibu ambao walimsaidia sana.[3]

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Mereba alizaliwa katika mji wa Montgomery, jimbo la Alabama tarehe 19 mwezi wa Septemba na mwaka wa 1990 kwa baba Mwethiopia na mama Mmarekani mweusi ambao walikutana wakati baba yake alikuja Marekani kusoma chuoni.[4] Kwa sababu wazazi wawili ni walimu wa chuo na walifundisha katika chuo kingine, familia yake walihama mara nyingi. Waliishi katika jiji la Philadelphia, jimbo la Pennsylvania, kisha mjini Greensboro jimbo la North Carolina, na baadaye jijini Atlanta jimbo la Georgia.[4] Pia, Mereba alikwenda nyumbani kwa baba yake katika nchi ya Ethiopia, jiji la Addis Ababa.[1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mereba alihitimu shule ya sekondari akiwa na miaka 17 na nia yake ya kwanza ilikuwa kuanza kazi ya muziki yake mara moja, lakini wazazi walimtaka yeye aende chuoni kwanza, hasa baba yake.[4] Yeye alikubali ombi lao, na alijiunga na Chuo kikuu cha Carnegie Mellon katika mji wa Pittsburgh. Halafu, alihama kutoka jimbo la Pennsylvania hadi jijini Atlanta kuenda Chuo kikuu cha Spelman kwa ajili ya kuwa karibu na kitovu cha muziki.[1] Ana shahada ya Kiingereza na Muziki.[4]

Shughuli za Muziki[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 2013, Mereba alianza shughuli yake ya rasmi na albamu yake iliitwa Room for Living, ambao ni muziki wa kitamaduni. Aliipa jina hilo kwa sababu alifanya muziki katika sebule yake. Baadaye, alianza kurekodi na studio ya kurekodi ya Red Kotton. Na Red Kotton, alitoa nyimbo kama "September" na "Radio Flyer" katika mwaka wa 2014, na EP fupi iliyoitwa Kotton House, Vol. 1 na studio ya kurikodi ya Jam Solutions. [2]

Baadaye, Mereba alianza kufanya kazi na Interscope Records katika mwaka wa 2018, na katika mwaka wa 2019 alitoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa The Jungle Is The Only Way Out, ambayo alifanya na wanamuziki wengine kama Ayo Olatunji na Sam Hoffman. Hoffman alifanya muziki na Mereba katika Room for Living na miziki mingine mingi baadaye, pia. [5]

Uvutano[hariri | hariri chanzo]

Mereba anasema alipenda muziki kutoka siku mama yake alipoleta albamu ya Bodyguard nyumbani wakati alipokuwa na umri wa 4.[4] Alianza kufanya muziki kwa kuimba, kisha alianza kuandika nyimbo kutoka shuleni. Anataja wanamuziki kama Whitney Houston, Stevie Wonder, Bob Marley, Tracey Chapman na watu kama hao kama wasani yake.[1][5]

Pia, Mereba anasema familia na marafiki zake walikuwa na msaada mkubwa. Binamu yake alimsaida kujifunza kuwa rapa, na yeye alivutia mvuto kwa Ethiopia. Alijifunza vitu mingi sana wakati alipotembelea familia huko. [1]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu Kamili[2]
Jina Albamu kwa kina
The Jungle Is The Only Way Out
●     Kuachiliwa: Februari 19, 2019

●     Studio ya kurikodi: Interscope

EP[2]
Jina Albamu kwa kina
Room for Living ●     Kuachiliwa: Februari 14, 2013

●     Studio ya kurikodi: Iliyotolewa mwenyewe

Kotton House, Vol. 1 ●     Kuachiliwa: Februari 10, 2017

●     Studio ya kurikodi: Jam Solutions/Remote Control Muziki

Nyimbo[2]
Jina Kuachiliwa
“September” Juni 3, 2014
“Radio Flyer” Juni 24, 2014
“Living on a Dream (feat. Doug E. Fresh)” Februari 28, 2017
“Black Truck” Februari 9, 2018
“Late Bloomer” Desemba 21, 2018
“Bet” Desemba 21, 2018
“Yo Love (From: “Queen & Slim:The Soundtrack”)” Novemba 11, 2019
“Same Boat (feat. Mereba)” - Kojey Radical Juni 11, 2020
“Heatwave (feat. JID) - Acoustic” Juni 19, 2020
“Golden pt. 2 (feat. Mereba)” – Berhana Novemba 11, 2020

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Andrea Dwyer (2014-09-16). INTERVIEW: Marian Mereba on her musical journey, her tree hugging ways & the Atlanta music scene (en-US). AFROPUNK. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 Mereba. Spotify. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.
  3. Patricia Ellah (2019-12-10). Urgently Necessary: An interview with Mereba. Teeth Magazine. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 Syreeta Martin (2016-07-22). Singer/Songwriter Marian Mereba (en-US). EBONY. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.
  5. 5.0 5.1 Steph Wong Ken (2020-02-14). Mereba and the Never-Ending Story of the Jungle (en). She Shreds Media. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.