Megan Smith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Megan J. Smith (alizaliwa 21 Oktoba 1964) [1] ni mhandisi na mwanateknolojia wa Marekani. Alikuwa Afisa Mkuu wa tatu wa Teknolojia wa Marekani (CTO ya Marekani) na Msaidizi wa Raisi,akihudumu chini ya Raisi Barack Obama . Hapo awali alikuwa makamu wa raisi wa Google, akiongoza maendeleo mapya ya biashara na ushirikiano wa hatua za awali katika timu za kimataifa za uhandisi na bidhaa za Google. Kwa miaka tisa, alikuwa meneja mkuu wa Google.org, [2] makamu wa raisi kwa muda mfupi ambapo alishirikiana kuunda WomenTechmakers, [3] ni Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Planet Out na alifanya kazi kwenye simu mahiri za mapema za General Magic . [4] [5] Anahudumu katika bodi za MIT [6] na Vital Voices, alikuwa mwanachama wa Kamati ya Ushauri ya USAID kuhusu Misaada ya Hiari [7] na alianzisha Mfuko wa Malala . [8] [9] Leo Smith ndiye Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa shift7. Mnamo Septemba 4, 2014, alitajwa kama wa tatu (na wa kwanza mwanamke) US CTO, akimrithi Todd Park, [10] [11] na kuhudumu hadi Januari, 2017.

Maisha ya mapema na elimu[hariri | hariri chanzo]

Smith alikulia Buffalo, New York, na Fort Erie, Ontario, [12]  na alitumia majira mengi ya kiangazi kwenye Taasisi ya Chautauqua huko Chautauqua, New York, ambapo mama yake, Joan Aspell Smith, alikuwa mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya Chautauqua. Smith alihitimu Shule ya City Honours mwaka 1982. [13] Aliendelea kupokea SB yake mnamo 1986 na SM mnamo 1988, ya uhandisi wa mitambo, kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts, na akamaliza kazi yake ya nadharia ya Uzamili katika MIT Media Lab . Alikuwa mwanachama wa timu ya wanafunzi wa MIT ambayo ilibuni, kujenga gari la mashindano linalotumia umeme wa jua takribani maili 2000 katika eneo la nje la Australia.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Smith aliolewa na mwandishi wa safu ya teknolojia Kara Swisher katika Kaunti ya Marin mnamo 1999 [14] (kabla ya kuhalalisha ndoa ya jinsia moja California). Wana watoto wawili wa kiume, Louis na Alexander, na wameachana. [15]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Megan Smith kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Megan Smith". Computer Hope. Iliwekwa mnamo October 3, 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "The Women at Google". 
  3. "Women Techmakers". 
  4. "Six who see the future". 
  5. "Do No Evil". Retrieved on 2022-03-17. Archived from the original on 2015-04-27. 
  6. "Corporation elects new members". MIT News. June 3, 2011. Iliwekwa mnamo October 3, 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. "ADVISORY COMMITTEE ON VOLUNTARY FOREIGN AID MEMBERS". USAID. 2013. Iliwekwa mnamo October 3, 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. "Introducing: The Malala Fund". 
  9. "Board of Directors". Vital Voices. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo October 6, 2014. Iliwekwa mnamo October 3, 2014.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  10. "White House names Google's Megan Smith the next Chief Technology Officer of the United States". 
  11. Howard, Alex (September 4, 2014). "Google[x] VP Megan Smith busts Silicon ceiling as first female US CTO". Tech Republic. Iliwekwa mnamo October 3, 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  12. Mabbett, Andy. "File:Megan Smith voice.flac". Iliwekwa mnamo 21 June 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  13. "Distinguished Alumni". City Honors School. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo October 6, 2014. Iliwekwa mnamo October 3, 2014.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  14. Wallace, Benjamin (15 July 2014). "Kara Swisher Is Silicon Valley’s Most Feared and Well-Liked Journalist. How Does That Work?". New York Magazine.  Check date values in: |date= (help)
  15. "Kara Swisher Biography and Ethics Statement". re/code. Iliwekwa mnamo July 31, 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)