Mayen Adetiba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mayen Adetiba
Amezaliwa 1954
Nigeria
Nchi Nigeria
Kazi yake maigizaji mwandishi wa habari

Maandishi ya italikiMayen Adetiba (alizaliwa mwaka 1954) ni mwigizaji,mwandishi wa habari na mhandisi wa nchini Nigeria.

Maisha Yake[hariri | hariri chanzo]

Adetiba alizaliwa mwaka 1954 nchini Nigeria..[1] Mwanzoni alitaka kuwa mhasibu lakini alivutiwa na uandishi wa habari.[2]

Alifanya kazi katika tamasha la Bar Beach Show na alikuwa mke wa Lakunle Ojo alipokuwa kijijini kwao.[2] Mayen alikwenda Marekani na kusoma katika chuo kikuu cha New York. Baadae aliambiwa kuwa uhandisi wa umeme unaweza kuthaminiwa zaidi barani Afrika kwa hivyo aliamua kubadili taaluma na kuhamia chuo kikuu cha columbia kusoma uhandisi wa umeme. Na aliendelea na masomo ya shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Cornell.[2]

Aliolewa na Dele Adetiba na kupata watoto wa tatu mmoja wa kike anayeitwa Kemi alizaliwa mjini Lagos mnamo Januari 1980[3]

Alichaguliwa kuwa Raisi wa chama cha Wahandisi wa Nigeria na alikuwa Makamu wa Rais wa Chama cha Wahandisi wa Nigeria mara tatu. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kwenye Kamati Kuu ya Jumuiya ya Wahandisi wa Nigeria.[3] Kazi yake ilikuwa inajumuisha kufanya kazi katika ofisi ya kanda ya Umoja wa Afrika Kusini iliopo nchini Malawi na kwenye kanisa kubwa la Summerhill Baptist la mjini Lagos. Hivi sasa anafanya kazi katika kampuni ya pro bono.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Admin (2016-08-22). "ADETIBA, Mayen Modupeola,". Biographical Legacy and Research Foundation (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-04-24. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "I set out to study accountancy, but graduated as an engineer –Adetiba". Punch Newspapers (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-04-24. 
  3. 3.0 3.1 "3 solid reasons why Kemi Adetiba's 'King of Boys' should NOT have been a hit". www.pulse.ng (kwa en-US). 2018-11-07. Iliwekwa mnamo 2020-04-24. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mayen Adetiba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.