Masaki (Dar es Salaam)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Slipway masaki

Masaki ni sehemu iliyopo Dar es Salaam katika wilaya ya Kinondoni.

Masaki kuna upepo mzuri kwa sababu sehemu hii ipo karibu na bahari, makazi yake yapo katika mpangilio wa mistari iliyonyoka, hivyo kufanya wakazi wa eneo hili kupata huduma mbalimbali kwa urahisi.

Watu wengi wanaoishi Masaki wana uchumi mzuri, wengi wao wamejiajiri na hivyo huwa na kipato kikubwa na kuboresha hali za maisha yao.

Wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali wanapofika Dar es Salaam hupenda kuishi Masaki kwa sababu ya mazingira safi na upepo mzuri wa bahari.