Mary Mgonja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mary Mgonja
Amezaliwa
Tanzania
Kazi yake mwanasayansi wa kilimo, mkurugenzi wa teknolojia


Mary Mgonja ni mwanasayansi wa kilimo kutoka Tanzania na mzalishaji wa mimea, pia ni mkurugenzi wa teknolojia na mawasiliano katika kampuni ya kilimo ya Namburi ya nchini Tanzania.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mary Mgonja ana shahada ya uzamivu katika falsafa na uzalishaji wa mimea. Shahada hiyo ameipata katika chuo cha Ibadani na International Institute of Tropical Agriculture.

Uzoefu wa kazi[hariri | hariri chanzo]

Mgonja amefanya kazi kama mwansayansi mkuu katika kuboresha kilimo cha ukame katika Taasisi ya Mazao sehemu zenye ukame katika maeneo ya Patancheru Hyderabad,Telangana nchini India.

Anaiwakilisha Tanzania katika Southern African Development Community (SADC) na East African Community (EAC). Pia amefanya kazi kama mkurugenzi wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) ambayo ni shirika linalosaidiwa na Bill and Melinda Foundation na Rockerfeller Foundation.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Citizen Correspondent (8 August 2016). "Body wants agriculture to go hi-tech". The Citizen. Dar es Salaam. Iliwekwa mnamo 22 November 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mary Mgonja kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.