Mariam Omar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mariam Omar
Chama Sauti ya Umma


Mariam Omar ni mwanasiasa wa visiwani Zanzibar, nchini Tanzania, ambaye ni mwanachama wa chama cha Sauti ya Umma (SAU).

Tarehe 30 Oktoba 2015, akiwa kama mgombea wa nafasi ya urais kutokea chama cha Sauti ya Umma, Mariam Omar alikuwa wa mwisho kati ya wagombea sita waliobaki, akipata asilimia 0.07 ya kura zote katika uchaguzi mkuu wa urais.[1] Alikuwa mwanamke wa kwanza kugombea nafasi ya urais visiwani Zanzibar.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ZANZIBAR PRESIDENCY ELECTION RESULTS. Tanzanian Affairs. Tanzanian Affairs. Iliwekwa mnamo 5 November 2010.