Mari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la milki ya Mari mnamo 2500 KK.

Mari (leo hii Tell Hariri nchini Syria) ilikuwa dola-mji wa ustaarabu wa Mesopotamia baina ya miaka 2900 - 1760 hivi KK.

Mji huo ulikuwa kando ya mto Frati, takriban katikati ya kitovu cha Mesopotamia na pwani ya Mediteranea na hivyo kitovu muhimu cha biashara ya kimataifa ya wakati ule.

Ulikuwa pia kitovu muhimu cha utamaduni na sanaa na kwa vipindi kadhaa ulitawala milki kubwa, ukishindana hasa na Ebla.

Katika mabaki yake yamepatikana maandishi mengi katika vigae.

Sanaa kutoka Mari[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mari kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.