Marcelo Vieira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Marcelo)
Marcelo Vieira.

Marcelo Vieira da Silva Junior (anayejulikana kama Marcelo; matamshi ya Kireno cha Brazil: [maʁˈsɛlu]; alizaliwa 12 Mei 1988) ni mchezaji wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na wa timu ya taifa ya Brazil. Anacheza kama beki wa kushoto na pia anaweza kucheza kama winga wa kushoto.

Mwaka 2005 alishinda taji la Campeonato Carioca akiwa na klabu ya Fluminense na mwaka 2006 alikuwa mchezaji bora wa Brazil akiwa na miaka 18 tu. Mwisho wa msimu huo alinunuliwa na Real Madrid kwa $ 8 milioni. Mpaka mwaka 2017 bado anacheza Real Madrid akiwa na magoli 28 akiwa amecheza mechi 408 amecheza misimu 11. Amebeba UEFA Champions Leagues mara tatu na ameshinda La Liga mara nne.

Ameichezea Brazil kwa mara ya kwanza 2006 dhidi ya Wales na akashinda goli na alikuwa mmoja wa timu ya Brazilkwenye michuano ya 2014 FIFA World Cup ambapo timu yao ilitoka kwenye ngazi ya nusu fainali na wakaitwa timu yenye ndoto za ubingwa.Na akaitwa timu bora ya msimu La Liga mwaka 2016.

Baada ya kumaliza msimu, Marcelo alisifiwa na magwiji wa soka kama Paolo Maldini na Diego Maradona ambaye alisema kuwa Marcelo ndiye mchezaji bora kwa nafasi yake. Na alianza kulinganishwa na Roberto Carlos ambaye alisema kwamba Marcelo ni mrithi wake, ni beki bora wa kushoto na akasema "Marcelo anacheza vizuri zaidi yangu".

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marcelo Vieira kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.