Manushi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Manushi ni kijiji kilichopo katika Kata ya Kindi, wilaya ya Moshi Vijijini katika mkoa wa Kilimanjaro.

Kijiji hiki kimetenganishwa na mto ambao unagawa sehemu mbili ambazo ni kijiji cha Kindi na kijiji cha Manushi.

Kijiji hicho kimekaliwa na wenyeji ambao ni Wachagga pamoja na wageni kutoka sehemu tofautitofauti. Wanakijiji wa Manushi hujishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo ni pamoja na Kilimo, Biashara n.k Kwa upande wa kilimo hujishughulisha na kilimo cha Ndizi, Mparachichi, Kahawa, Viazi na Maharage kama vyakula vyao vikuu.

Kwa upande wa hali ya hewa Manushi huwa na hali nzuri ya ubaridi na upepo mwanana, ambao wenyeji hupenda hali hiyo. Pia wenyeji na wageni wa Manushi hupenda kunywa kahawa asubuhi kutokana na hali ya hewa kuwa na baridi, hivyo kahawa ndiyo kinywaji chao kikuu.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Manushi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.