Mamy Baby
Mkuwe Isale (anajulikana kama Mamy Baby; amezaliwa Tabora, Novemba 12, 1989) ni mtangazaji wa redio na mwanahabari kutoka Tanzania. [1] [2] [3] [4] [5] [6]
Isale alizaliwa kwenye familia ya kichifu ya Wanyamwezi, Fundikira. [7] [8] Alianza elimu yake rasmi katika Shule ya Msingi Isike na baadaye akajiunga na Shule ya Sekondari ya Kazima. Akiongozwa na shauku ya mawasiliano na kusimulia hadithi, aliamua kusoma uandishi wa habari, na kupata Diploma ya Juu kutoka Chuo cha Royal cha Uandishi wa Habari. Msingi huu wa taaluma yake katika media ndio chanzo cha kazi yake katika vyombo vya habari na zaidi.. [9]
Maisha ya binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Desemba 30, 2022, Mamy Baby alisherehekea tukio muhimu katika maisha yake binafsi kwa kufunga ndoa na Dk. Hassan Abbas, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania . [10] [11] [12] Dk Hassan Abbas kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania. [13] [14] [15]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Kazi ya Mamy Baby katika vyombo vya habari ilianza mwaka 2009 mjini Arusha, ambapo alifanya kazi katika Mambo Jambo (MJ FM). Shauku yake ya redio ilimpelekea kujiunga na Radio 5, ambapo alifanya kazi kuanzia mwaka 2011 hadi 2013. Mnamo mwaka 2013, alijiunga na East Africa Radio, ambapo alihost kipindi cha The Cruise pamoja na Sam Misago na DJ Sinyorita hadi mwaka 2015.
Mnamo mwaka 2016, Mamy Baby alihamia Clouds FM, ambapo alikua sehemu ya timu ya XXL, kipindi bora cha burudani katika kituo hicho. [16] Pamoja na B Dozen, Adam Mchomvu, na KenedyTheRemedy, [17] alendelea kujenga sifa yake kama mmoja wa sauti zinazotambulika zaidi katika redio ya burudani nchini Tanzania.. [18]
Mchango na Ushawishi
[hariri | hariri chanzo]Clouds FM, Mamy Baby amekuwa na mchango mkubwa katika kuutangaza muziki na utamaduni wa Kitanzania. Mamy anaendelea kuleta mabadiliko kupitia DADA HOOD, mpango wake unaojitolea kuwatia moyo na kuwaelekeza wasichana Vijana. [19] [20] [21] [22]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Clouds FM Top 20: List ya midundo 20 ya wiki, leo January 21, 2018 - Millard Ayo" (kwa American English). 2018-01-21. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ "CloudsFM Top 20: Ngoma 20 kali zilizopangwa kwenye list leo April 2 - Millard Ayo" (kwa American English). 2017-04-02. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ "BMT | DADA HOOD KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUINUA MICHEZO YA WANAWAKE". www.bmt.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ Yahu, Joel (2024-02-16). "AUDIO Rosa Ree Ft Chemical X Frida Amani X S2kizzy X Mamy Baby (Dada Hood) - Naona Love MP3 DOWNLOAD — citiMuzik" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ DADA HOOD NAONA LOVE ROSA REE X CHEMICAL X FRIDA AMANI X S 2 KIZZY X MAMY BABY, iliwekwa mnamo 2024-09-30
- ↑ Digital, Mtanzania (2017-06-24). "DADA HOOD; ILIKUWA BONGE LA CHEMISTRY AISEE!". Mtanzania (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ "Tribute To Chief Fundikira". venansioahabwe.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-10-08.
- ↑ Rockel, Stephen J. (Juni 2019). "The Tutsi and the Nyamwezi: Cattle, Mobility, and the Transformation of Agro-Pastoralism in Nineteenth-Century Western Tanzania". History in Africa (kwa Kiingereza). 46: 231–261. doi:10.1017/hia.2019.5. ISSN 0361-5413.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "MamyBaby". Music In Africa (kwa Kiingereza). 2022-11-19. Iliwekwa mnamo 2024-10-08.
- ↑ "Dkt. Hassan Abbas Afunga Ndoa na Mtangazaji wa Clouds Mamy Baby – Video". Global Publishers (kwa American English). 2022-12-30. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ "Dk Abbas afunga ndoa na Mamy Baby wa Clouds - HabariLeo" (kwa American English). 2022-12-30. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ "Dk Hassan Abbas katibu mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-10-02.
- ↑ "Dkt. Abbas katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-10-02.
- ↑ "President Samia makes changes in cabinet and regional administration". The Citizen (kwa Kiingereza). 2023-02-26. Iliwekwa mnamo 2024-10-02.
- ↑ "Habari | Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa". www.modans.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-10-02.
- ↑ "XXL ya Clouds FM yafunga mwaka na Wanavyuo Tanzania – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-10-02.
- ↑ "Mama alinifundisha maisha, namna ya kuwajali wanawake wengine – Jux – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-10-02.
- ↑ "Vuta N'kuvute: Dj Sinyorita na Mami wa EA Radio wachukuliwa na... – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ "SIKU YA WANAWAKE Warembo wanavyoupiga mwingi Bongo | JAMHURI MEDIA". www.jamhurimedia.co.tz (kwa American English). 2022-03-08. Iliwekwa mnamo 2024-10-02.
- ↑ zanzinews.com. "Wasanii wa Kike Dada Hood,BMT Kuunga Mkono Juhudi za Rais Mhe. Samia Suluhu Kusaidia Michezo Nchini". ZanziNews. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ mzalendoeditor (2022-02-23). "WASANII WAKIKE, DADAHOOD, BMT KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUSAIDIA MICHEZO NCHINI". Mzalendo (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-09-30.
- ↑ "News |MINISTRY OF CULTURE ARTS AND SPORTS". www.michezo.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-09-30.