Malinyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Malinyi ni kata ya Wilaya ya Malinyi katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67619.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 31,249 [1] walioishi humo.

Wakazi wa kata hii wanajishughulisha na kilimo cha mpunga. Mwaka 2012 shirika la umeme wa mwanga wa jua <TAREA> lilianza kusambaza umeme huo mji mzima.

Kuna shule za sekondari tano; shule hizo ni shule ya sekondari Malinyi, shule ya sekondari Kipingo, Shule ya sekondari Tira, shule ya sekondari Tumaini na shule ya sekondari Mtakatifu Pius.

Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika, kuna shule za msingi tano, nazo ni: shule ya msingi Nawigo, shule ya msingi Malinyi, shule ya msingi Makugira, shule ya msingi Makaerere na shule ya msingi Kipingo.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Morogoro - Ulanga DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-04.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Malinyi - Mkoa wa Morogoro - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Biro | Igawa | Itete | Kilosa Mpepo | Malinyi | Mtimbira | Ngoheranga | Njiwa | Sofi | Usangule


Ramani Wilaya au manisipaa Wakazi (2002) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Wilaya za Mkoa wa Morogoro
Wilaya ya Kilombero 321,611 5 19 81 14,918
Wilaya ya Kilosa 489,513 9 37 164 14,245
Wilaya ya Morogoro Vijijini 263,920 6 25 132 11,925
Wilaya ya Morogoro Mjini 227,921 1 19 - 531
Wilaya ya Mvomero 260,525 4 17 101 7,325
Wilaya ya Ulanga 193,280 5 24 65 24,560
Jumla 1,759,809 30 141 543 73,039
Makisio ya idadi ya watu kwa mwaka 2008 ni watu 2,021,714
kutokana na kiwango cha ongezeko la watu la asilimia 2.6 kwa mwaka.
Marejeo: Mkoa wa Morogoro
Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malinyi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.