Nenda kwa yaliyomo

Rasi ya Malay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Malay Peninsula)
Rasi ya Malay
Rasi ya Malay

Rasi ya Malay (Kimalay: Semenanjung Tanah Melayu) ni rasi kubwa katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Ina pande tatu:

  • Kaskazini-magharibi yake ni eneo la kusini kabia ya Myanmar (Burma)
  • Katikati yake ni eneo la Uthai
  • Kusini ni eneo la Malaysia ya magharibi

Kusini kabisa iko Singapor kwenye kisiwa karibu na ncha ya rasi

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Rasi ya Malai iko kati ya Bahari Hindi na Pasifiki. Upande wa Pasifiki ni Ghuba ya Uthai na Bahari ya Uchina. Mlango wa Malakka unatenganisha rasi na kisiwa cha Sumatra

Rasi inaanza kwenye latitudo ya +13 na kuelekea kusini hadi latitudo ya +1. Urefu wake ni 1,555 km. Sehemu nyembamba iko katika sehemu ya Kithai yenye 60 km pekee.

Sura ya nchi ina tabia mbalimbali: milima, tambarare, maziwa, pwani na misitu minene.

Milima ya juu ni Gunung Tahan (2,187 m) hohe Gunung Korbu (2,184 m) nchini Malaysia. Katika tambarare za Uthai iko Khao Luang (1,786 m). Sehemu ya Myanmar kuna Recho Taung (1,330 m).

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Malay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.