Nenda kwa yaliyomo

Makazi ya kuhifadhi wanyama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya mbwa aliyeko kwenye makazi ya kuhifadhi wanyama Washington, Iowa.
Paka akiwa kwenye makazi ya kuhifadhi wanyama.

Makazi ya kuhifadhi wanyama ni mahali ambapo wanyama waliopotea, walioachwa, hasa mbwa na paka, na wakati mwingine wanyamapori majeruhi au wagonjwa huhifadhiwa na kutibiwa.

Ingawa kuna makazi yasiyoruhusu wanyama kuuliwa, wakati mwingine sera ya kuua wanyama wagonjwa au wanyama wasiochukuliwa haraka na wamiliki wao hutumika. Huko Ulaya, nchi 30 zilijumuishwa kwenye utafiti, ni nchi nne tu ambazo zinaruhusu mauaji ya mbwa wenye afya waliopotea. Nchi hizo ni Ucheki,[1] Ujerumani, Ugiriki na Italia.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "246/1992 Coll. LAW Czech National Council to protect animals against cruelty (paragraph 13)". portal.gov.cz. Iliwekwa mnamo 2017-01-03.
  2. World Society for the Protection of Animals & The Royal Society for the Prevention of Cruelty to Animals International (2007). Report Stray Animal Control practices (Europe) An investigation of stray dog and cat population control practices across Europe. uk. 18.