Majadiliano ya mtumiaji:Nathan Baraka
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
CaliBen (majadiliano) 13:15, 21 Mei 2021 (UTC)
Nathan habari, umejaribu kutunga makala kuhusu mto Mbofwe lakini kwa bahati mbaya umeharibu makala ya mto Mto Idodi. Nimefuta kayi zako. Tafadhali uelewe: 1) ni marufuku kuandika juu ya kazi ya mtu mwingine ukitaka kujadili jambo tofauti. 2) Ukipenda kuchangia anza kuwa makini zaidi usilete Kiswahili kibaya kama "Mto mbofwe", maana "Mbofwe" ni jina na majina huandikwa kwa herufi kubwa mwanzoni. 3) usitumie sana alama za herufi koze ''' katika matini. Herufi koze ni kwa kichwa cha makala, yaani maneno ya kwanza pekee. Tumia muda kusoma Wikipedia:Mwongozo. 4) katika Mwongoze utafute utaratibu wa kuweka viungo vya ndani kwa kutumia mabano mraba [[...]]. 5) Kabla kuleta mada hapa utafute vyanzo, yaani tovuti au vitabu vinavyothibitisha ukweli wa yale unayotaka kueleza. Angalia Mwongozo kuhusu Vyanzo. 6) Halafu naomba sana uitikie na kuthibitisha hapa kwamba umesoma maelezo yangu. Ili tuweze kushirikiana tafadhali uandike hapo chini kwamba umeelewa, menginevyo inaweza kutokea kwamba utazuiliwa kuingia. Ukipenda kuanzisha makala kuhusu mto Mbofwe, tafadhali utafute chanzo kwanza. Uniandikie nitakusaidia jinsi ya kutunga. Kipala (majadiliano) 17:43, 23 Mei 2021 (UTC)
Makala za vitongoji na vijiji katika Mufindi
[hariri chanzo]Nilipaswa kufuta makala hizo. Sijaona muundo unaofaa. Katika makala ya vijiji uliorodhesha 18, lakini ziko 50 au zaidi, nikitazama orodha ya posta. Kama ungeweza kuorodhesha vyote ungeweza kuyaweka katika makala za Kata kwenye Wilaya ya Mufindi. Kazi hii nimefanya kwa Kasanga (Mufindi), maana haina faida kutawanya elimu mno kwa kugawa kila kitu hadi makala za pekee kama hatuna habari zaidi kuhusu vijiji na vitongoji. Kama habari ziko, tunaweza kuanzisha makala ya pekee. Lakini haisaidii tukitunga makala ya maneno matano inayotaja vijiji vitano tu bila habari ya ziada. Pia naomba angalia Wikipedia:Mwongozo. Kila makala inahitaji jamii, na kuweka viungo vya ndani. Ukiwa na swali, karibu!Kipala (majadiliano) 20:05, 23 Mei 2021 (UTC)