Majadiliano ya mtumiaji:Maria alphonce

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Habari dada Maria Alphonce! Umeona kwamba hapa ndipo penyewe eeeehh! Karibu sana na ni furaha yetu kuona wachangiaji wapya kwenye mradi huu. Haya, kuwa huru kuandika makala uzipendazo, dada yangu. Makala za Wikipedia zina mwenendo wake. Ili kujua mwenendo huo, tafadhali fungua hapa. Karibu sana. Nikiwa ninatokea Dar es Salaam, Tanzania, niite Muddyb au,--Muddyb MwanaharakatiLonga 16:20, 22 Novemba 2009 (UTC)

Salam. Umeona kwamba nimeongeza kitu kama INTERWIKI. Tazama hapa utaonam nimeweka viungo vya INTERWIKI (viungo vya makala ileile kwenda kwa lugha nyingine kama vile Kiingereza, Kijerumani, Kirusi, nk. Si kazi ngumu sana, lakini makala imepiga hatua! Ongeze juhudi.--Muddyb MwanaharakatiLonga 16:39, 22 Novemba 2009 (UTC)
Salaam na karibu pia kutoka kwangu! Naomba uangalie Majadiliano:Riwaya ya Blindness ni machache kuhusu umbo la makala hii --Kipala (majadiliano) 15:04, 9 Desemba 2009 (UTC)

Muundo wa makala[hariri chanzo]

Dada, salam! Unaombwa utupie macho angalau kwenye ukurasa wa Wikipedia:Mwongozo - utakusaidia katika uhandishi wako. Vinginevyo, utakuwa unachekesha watu walionuna! Makala ya Joshua Nkomo haijafuata taratibu za Wikipedia kabisaaa! Hibyo, unaombwa utumie muda kidogo wa kujisomea kwenye ukurasa wa mwongozo! Karibu sana.--Muddyb MwanaharakatiLonga 17:08, 14 Desemba 2009 (UTC)

Makala ya Edger Luhende Ngelela[hariri chanzo]

Maria, umeandika makala ndeefu bila hata kutaja marejeo au vyanzo. Hii kuna uwezekano mkubwa wa kufutwa. Pia, makala haijafuta muundo wa makala za wikipedia - ipo hovyo-hovyo. Unaombwa usahihishe, dada.--Muddyb MwanaharakatiLonga 15:04, 18 Desemba 2009 (UTC)

Salam, Maria. Umeona kwamba ni afadhali utumie muda wako kujipatia uzoefu eeh?? Basi umefaulu kuiweka sawa makala hii ya Edger. Tena hata ile ya Blindness nayo ipo poa sana, dada yangu. Kumbe unajua, ila tu mbwembwe nyiingi hadi basi. Ukiendelea hivi, tegemea kupata rundo la maksi. Kingine: Nimeona umepakiza picha ya wapendano halafu ukasema ni leseni huria ya umma, lakini cha kushangaza hujasema umeitoa wapi? Kwa picha, bado itaendelea kuwa mtihani kidogo dada yangu. Wako,--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:57, 21 Desemba 2009 (UTC)

makala zihitajizo habari[hariri chanzo]

Dada Maria, salaam! Wakati wa shindano, makala nyingi zimeanzishwa bila kuwekewa yaliyomo hata kidogo, nasi wanawikipedia hatukuwa na nafasi ya kurekebisha sana. Kwa hiyo sasa, naomba tusaidiane kusawazisha hizo makala. Kwa mfano, ungeweza kuanza kwa kuangalia orodha ya makala bila jamii. Bila shaka utagundua kadhaa ambazo ni duni, labda yenye maneno mawili matatu tu. Ndivyo nilivyogundua k.m. na makala ya Henri Fayol, mhandisi Mfaransa wa karne ya 19. Sasa ukiangalia mabadiliko niliyoyaingiza utapata mambo ya msingi ya wikipedia. K.m. naingiza kigezo cha {{DEFAULTSORT}} kwa ajili ya orodha ya makala katika jamii ifuate alfabeti vizuri. Tena naingiza jamii za miaka ya kuzaliwa (k.m. [[Jamii:Waliozaliwa 1841]]) na ya kufariki (k.m. [[Jamii:Waliofariki 1925]]). Pia, ikiwa ni makala fupi bila maelezo mengi, naingiza kigezo cha {{mbegu-mtu}} (yaani kama ni mtu). Hatimaye, naingiza kiungo kwa wikipedia ya Kiingereza (k.m. [[en:Henri Fayol]]) ambapo naweza kupata code kwa picha ya mtu (k.m. [[Image:Fonds henri fayol.jpg|thumb|right|Henri Fayol]]) pamoja na habari nyingine. Nitashukuru kwa msaada wako katika kuboresha makala mpya zilizoachwa duni. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 10:59, 2 Februari 2010 (UTC)


Asante sana Baba Tabita.

Nashukuru kwa kupata barua pepe kutoka kwako. Nimejaribu kuangalia baadhi ya makala kati ya zile ulizoziorodhesha, ni kweli kwa kiasi kikubwa zinaonesha kukoso vitu muhimu au muundo wa makala za wiki, kama ulivoainisha baadhi ya vitu vinavyokosekana katika makala hizo.

Nitahidi kutoa msaada wangu kwa kile kiasi kidogo ninachokiweza, na pia nategemea kupata ushirikiano kutoka kwenu.

Lakini kwa sasa najiandaa na mitihani ya chuo, ya nusu muhula itakayoanza tarehe nane mwezi huu, kwa sababu hiyo, nitabanwa na masomo kwa kiasi fulani, lakini baada ya hapo nitakua likizo kwa kiasi cha wiki nne au tano , hivyo nategemea kutumia muda huo wka ajili ya wikimakala.--Maria alphonce (majadiliano) 15:00, 3 Februari 2010 (UTC)

Asante sana, Maria, kwa jibu lako. Naelewa mabano ya mitihani nami nakutakia mafanikio mema. Pia nimefurahi kusikia kuwa una nia ya kuendelea na wikipedia. Unisamehe nikiendelea kuandika kuhusu usafishaji wa wikipedia baada ya shindano. Sababu hasa ni kwamba tukiendelea kuboresha makala zilizoongezeka, tuwe makini. Kabla hatujaongeza au kurekebisha habari za makala fulani, lazima tuangalie majadiliano na ukurasa wa historia ya makala hiyo. Angalia k.m. makala ya uchumi. Ukiihariri bila kuangalia majadiliano yake wala historia yake, inawezekana utaongeza kazi ya baadaye kwa vile tafsiri za shindano zilizofuta makala za zamani (pamoja na jamii na interwiki zake) hazijaunganishwa. Nitaendelea kutafuta makala kama hiyo na kuziandikia katika majadiliano yake. Kwa ajili ya kuunganisha tafsiri mbili au zaidi, labda itasaidia ukifungua zote, kila moja katika dirisha lake, na kunakilisha sehemu za makala za zamani kwenda katika makala ya sasa. Pole na kazi. Na asante kwa kazi yako. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 04:11, 4 Februari 2010 (UTC)

Salam, good afternoon![hariri chanzo]

Sorry to bother you, I apologize sincerely I don't speak Swahili so I hope you'll forgive me for using English. My name is Claudi Balaguer (User Capsot from the Catalan and Occitan Wikipedias) and I'm currently working on a campaign to help our association "Amical de la Viquipèdia" in order to be accepted as a Chapter (an intermediate superstructure between the Wikimedia Foundation and the Wikipedias), demand which hasn't been accepted until now because Catalan is not a/one state language. I think you understand very well what it is to speak a minorized language, to strive to protect and preserve it and I hope you will think our cause is just since it might open the door to all the minorized or stateless languages which can't currently apply for a Chapter even though they might be organized and working hard! In order to support us, you can paste the following template Wikimedia CAT in your userpage and/or sign the link of the template. Asante for your attention, I wish you a pleasant, sunny and warm summertime, take care, Capsot (majadiliano) 12:25, 17 Agosti 2010 (UTC)

makala kuhusu wanafalsafa[hariri chanzo]

Maria, salaam! Nimefurahi sana kuona makala ulizoziandika (au kutafsiri?) kuhusu wanafalsafa hasa kutoka Ufaransa. Hongera sana! Nimehuisha viungo vya tarehe za kuzaliwa na kufariki na kuziingiza kwenye kurasa za tarehe na miaka. Tusonge mbele! Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 13:13, 20 Desemba 2011 (UTC)

Karibu tena![hariri chanzo]

Karibu tena, Maria. Muda sasa tangu ulivyoianza safari. Ukiona ya kwamba unahitaji msaada, tafadhali utujulishe tu na tutakusaidia!--MwanaharakatiLonga 17:04, 2 Januari 2012 (UTC)