Madaktari wasio na Mipaka-MSF
Madaktari wasio na Mipaka (linajulikana mara nyingi kwa jina lake la Kifaransa Médecins Sans Frontières au kifupi chake MSF) ni shirika lisilo la serikali la kimataifa.
Ni maungano ya madaktari na wauguzi pamoja na wasaidizi wengine wanaojitolea kuwasaidia wagonjwa katika maeneo pasipo na huduma za kiafya hasa katika nchi penye vita za wenyewe kwa wenyewe au maafa asilia.
Shirika la MSF lilianzishwa 1971 na kundi la madaktari Wafaransa (kati yao Bernard Kouchner) baada ya vita ya Biafra huko Nigeria.
MSF hutawaliwa siku hizi na kamati ya wakurugenzi wanaokutana kwenye makao makuu mjini Geneva (Uswisi). Kila mwaka takriban madaktari na wauguzi 3,000 waingia katika miradi mbalimbali kwenye nchi 70 na wengi wao hukitolea wakati wa likizo bila malipo yoyote. Kuna waajiriwa takriban 1,000. Makisio ya mwaka hufikia jumla la dola za Marekani milioni 400 na asilimia 80 zachangiwa kwa njia ya zawadi za watu wa binafsi. Inayobaki ni pesa za serikali mbalimbali au shirika za kimataifa kama UM au Umoja wa Ulaya.
Mifano ya miradi ya MSF ni mahali kama Kosovo wakati wa vita, Sudan ya Kusini, Darfur, Chechniya au maeneo yaliyoathiriwa na tsunami ya Bahari Hindi mwaka 2004.
MSF ilipokea tuzo ya Nobel ya Amani mwaka 1999.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Médecins Sans Frontières International
- Official Nobel Peace Prize page for MSF Ilihifadhiwa 7 Agosti 2004 kwenye Wayback Machine.
- Essentialdrugs.org
- Observatoire de l'action humanitaire Ilihifadhiwa 9 Mei 2005 kwenye Wayback Machine.
- Drugs for Neglected Diseases Initiative
Matawi ya MSF
[hariri | hariri chanzo]- Médecins Sans Frontières Australia
- Médecins Sans Frontières Canada / Doctors Without Borders Ilihifadhiwa 24 Januari 2013 kwenye Wayback Machine.
- Médecins Sans Frontières UK Ilihifadhiwa 3 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine.
- Médecins Sans Frontières USA / Doctors Without Borders
- Aid Watch Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Intelligent Giving profile of MSF UK Ilihifadhiwa 17 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.