Nenda kwa yaliyomo

McDonald Mariga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka MacDonald Mariga)
McDonald Mariga
Maelezo binafsi
Jina kamili McDonald Mariga Wanyama
Tarehe ya kuzaliwa 4 Aprili 1987
Mahala pa kuzaliwa    Nairobi, Kenya
Urefu 187 cm
Timu ya taifa
2006- Kenya

* Magoli alioshinda

McDonald Mariga Wanyama (amezaliwa 4 Aprili 1987) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Kenya. Baada ya kustaafu, ameingia katika siasa.

Wasifu wa klabu

[hariri | hariri chanzo]
McDonald Mariga

Mariga alianza kucheza kambumbu na timu ya Ulinzi Stars kabla kuhamia timu ya Pipeline FC. Mariga alikuwa mojawapo wa wachezaji wa timu ya 'Golden Boys' katika shule ya upili ya Kamukunji. Alishirikiana humo na mwenzake katika timu ya taifa ya Kenya Dennis Oliech ambaye anachezea klabu ya Auxerre, Ufaransa. Timu yao ya 'Golden Boys' ilishinda Kombe la Mabingwa wa Taifa miaka miwili mfululizo (2002 na 2003).

Alikuwa mchezaji wa kati ya uwanja huku akishirikiana na wenzake kufikisha mpira kwa washambuliaji. Aliendelea na jukumu hili katika timu alipohamia Uswidi kucheza katika timu ya Enköpings SK. Baada ya msimu mmoja tu ya kuwa Enköpings aliajiriwa na timu ya Helsingborgs IF kabla msimu wa 2006. Alifanikiwa mjini Olympia kwa haraka sana.[1] Meneja maarufu kutoka timu ya Portsmouth, Harry Redknapp, alikuwa akimtaka achezee timu yake katika ligi ya Uingereza. Mariga alionekana kuelekea kuchezea timu hiyo lakini matatizo ya kupata kibali cha kazi yalimkumba na mpango huo kutofaulu. Gharama ya ubadilishaji wa huduma zake Mariga kutoka Helsinborg hadi Portsmouth ulikisiwa kuwa euro milioni 2.7.

Alihamia ligi ya Serie A akichezea klabu ya Parma FC kwa mpango wa aina ya mkopo katika mwezi wa Agosti 2007. Timu hiyo ya Kiitaliano ilikuwa na nafasi ya kumnunua kwa ada ya Kronor ya Uswidi milioni 20. Mariga alikubali kuajiriwa kwa miaka minne na klabu ya Parma hadi mwisho wa Juni 2012 baasa ya klabu hiyo kulipa ada ya uhamisho wa Kronor ya Uswidi milioni 18(takriban euro milioni 1.94). Mpango huo ulioandaliwa na aliyekuwa mchezaji maarufu wa Uswidi Martin Dahlin, ilikuwa na gharama iliyokuwa chini ya bei ya awali ya Kronor ya Uswidi milioni 20 iliyowekwa na Helsinborg. 25% ya ada ya uhamisho ulikwenda kwa Enkopings SK, ambayo ilkuwa klabu iliyompeleka Mariga Uswidi mnamo mwaka 2005.

Mariga ambaye huduma zake zilikuwa zimekadiriwa kuwa na thamani ya euro milioni 0.8 mnamo Julai 2008 lakini sasa amemea katika mchezo akawa mahiri zaidi. Hii imesababisha thamani yake kuongezeka pole pole hadi euro milioni 1.94 baada ya mwaka mmoja tu. Amecheza vizuri sana katika ligi ya Kiitalia ya Serie A tangu kuhama Helsinborg huku akiwa mmojawapo wa vijana waliokua kwa haraka sana katika klabu hiyo.

Mariga alichezea timu ya Parma mara 35 katika ligi ya Serie B wakati wa msimu wa 2008-2009 huku akifunga mabao matatu ili kuwasaidia kurudi ligi ya Serie A kwa msimu wa 2009-2010.

Wasifu wa Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Mariga alifunga bao lake la kimataifa la kwanza dhidi ya Swaziland tarehe 25 Machi 2007.

  1. "McDonald Mariga". SvFF. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-26. Iliwekwa mnamo 2009-05-17.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu McDonald Mariga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.