Ulinzi Stars

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ulinzi Stars ni klabu ya Kenya iliyo na makao yake katika mji wa Nakuru.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ulinzi Stars ni klabu inayohusishwa na Jeshi la Kenya huku wachezaji wao wengi wakiwa wanajeshi. Wao hushindana katika ngazi ya juu ya ligi, Ligi Kuu ya Kenya. Timu hii imekuwa mabingwa wa Kenya mara tatu; mwaka wa 2003,wa 2004, na wa 2005 . Hii ilifanya kuwa timu ya tatu katika Ligi Kuu ya Kenya kuwa mabingwa kwa miaka mitatu mfululizo, baada ya AFC Leopards na Gör Mahia. Ulinzi Stars hucheza mechi zao katika Uwanja wa Afraha,[Nakuru]. Hapo zamani, makao ya klabu hiyo ilikuwa katika mji wa [Thika], lakini imehamia mji wa [Nakuru] tangu msimu wa 2004/05.Mechi zao zote za nyumbani wamekuwa wakicheza katika Uwanja wa Afraha, [Nakuru].

Ulinzi Stars pia ndio timu ya Jeshi La Kenya na wamehitimu kucheza katika Mashindano Ya Majeshi Duniani ya mwaka wa 2011.

Mbali na kuwa na timu ya soka,walikuwa na timu ya mpira wa vikapu iliyoitwa Ulinzi Warriors.Ulinzi Warriors iliacha kucheza mwaka wa 2007 ingawa walikuwa Mabingwa watetezi katika ligi ya mpira wa vikapu.Timu hii ilikuwa imeshinda ligi hiyo ya mpira wa vikapu mara tano mfululizo.Palikuwepo pia na timu za raga na voliboli.

Utendaji katika mashindano ya CAF.[hariri | hariri chanzo]

Ligi ya Mabingwa ya CAF 2004: Ilijitoa katika raundi ya kwanza

Utendaji katika Ligi Kuu katika Msimu wa 2009[hariri | hariri chanzo]

Thika United	 1-0 Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  0-0 Nairobi City Stars
Ulinzi Stars	  1-1 Mathare United FC
Western Stima	  1-1	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  2-1 Bandari F.C.
Tusker	      0-0	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  0-2 AFC Leopards
Ulinzi Stars	  2-1 Agro-Chemical
Gor Mahia	  4-2	Ulinzi Stars
Sony Sugar	  1-0	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  0-0 KCB
Sher Karuturi	  0-1	Ulinzi Stars
Chemelil Sugar   1-3 Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  0-0 Sofapaka
Red Berets F.C.   0-0 Ulinzi Stars
Mathare United FC  2-2 Ulinzi Stars
Bandari F.C.	  1-1	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  2-2 Western Stima
AFC Leopards	  1-1	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  2-1 Chemelil Sugar
Ulinzi Stars	  0-2 Tusker
Nairobi City Stars 0-0 Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  0-0 Sony Sugar
Agro-Chemical	  0-1	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  0-0 Thika United
Ulinzi Stars	  2-0 Sher Karuturi
KCB	      2-0	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  0-0 Red Berets F.C.
Sofapaka	  2-0	Ulinzi Stars
Ulinzi Stars	  1-0 Gor Mahia

Wachezaji bora wa Ulinzi Stars Geoffrey Kokoyo,Hillary Echesa,Nyongesa Barasa,Lawrence Owino na Evans Amuoka ni wachezaji wa Ulinzi Stars waliocheza katika timu ya taifa hasa katika mashindano ya CECAFA ya 2009. Anayejulikana zaidi ni golikipa aliyelinda lango kwa timu ya Ulinzi Stars na timu ya taifa pia: Francis Onyiso.

Viungo vya nje