Haramia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Created page with 'thumb|250px|Bendera ya kihistoria ya maharamia Wazungu kwenye [[Atlantiki ]] '''Haramia''' ni jambazi anayefanya mambo yake kwenye gi…'
 
jamii
Mstari 12: Mstari 12:
Wakati mwingine maharamia walitawala pia maeneo ya mabandari walipokuwa na kimbilio chao kama [[dola-mji]]. Mfano mashuhuri wa madola haya madogo ilikuwa [[jamhuri ya Bou Regreg]] katika [[Moroko]] ya leo wakati wa karne za 17-19.
Wakati mwingine maharamia walitawala pia maeneo ya mabandari walipokuwa na kimbilio chao kama [[dola-mji]]. Mfano mashuhuri wa madola haya madogo ilikuwa [[jamhuri ya Bou Regreg]] katika [[Moroko]] ya leo wakati wa karne za 17-19.


[[jamii:Uharamia]]
[[Jamii:Sheria]]


[[ar:قرصنة]]
[[ar:قرصنة]]

Pitio la 13:24, 15 Aprili 2009

Bendera ya kihistoria ya maharamia Wazungu kwenye Atlantiki

Haramia ni jambazi anayefanya mambo yake kwenye gimba la maji hasa baharini.

Kufuatana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya sheria za bahari uharamia ni matendo ya jinai yoyote yanayotekelezwa baharini na mabaharia au maabiria wa wa meli au ndege ya binafsi dhidi ya meli au ndege nyingine au dhidi ya watu na mali kwenye chombo cha aina hii.

Katika historia maharamia wamejulikana tangu habari za kwanza juu ya usafiri kwenye bahari. Kati ya habari za kwanza ni zile kuhusu maharamia kwenye Mediteranea mnamo karne ya 13 KK.

Julius Caesar alipokuwa kijana alikamatwa na maharamia akaachichwa nao baada ya malipo ya ufidiwa mkubwa baadaye akarudi akalipiza kisasi na kuwaua maharamia.

Siku hizi eneo lenye uharamia mbaya ni Indonesia lakini ni hasa maharamia wa Somalia walioonekana sana katika habari tangu mwaka 2008.

Wakati mwingine maharamia walitawala pia maeneo ya mabandari walipokuwa na kimbilio chao kama dola-mji. Mfano mashuhuri wa madola haya madogo ilikuwa jamhuri ya Bou Regreg katika Moroko ya leo wakati wa karne za 17-19.