Lusia wa Sirakusa
Mandhari

Lusia wa Sirakusa (maarufu kama Mtakatifu Lusia; 283 – 304) alikuwa msichana bikira na tajiri wa Siracusa, Sicilia, Italia visiwani ambaye alitetea imani yake ya Kikristo hadi kuuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano.
Kadiri ya Injili, maisha yake yote alitunza taa yake inawaka ili kumlaki Kristo, Bwanaarusi wake, akamfia na kuingia pamoja naye kwenye arusi ya mbinguni, akafurahie milele nuru isitotua kamwe [1].
Anachorwa akishika mkononi sinia yenye macho yake aliyonyofolewa kabla hajauawa.
Kwa sababu hiyo anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Desemba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 446-447
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 387
- Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 95
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Jacobus de Voragine, Legenda Aurea: Ilihifadhiwa 9 Desemba 2000 kwenye Wayback Machine. St. Lucy (e-text, in English)
- "Cara Santa Lucia..." Ilihifadhiwa 9 Desemba 2013 kwenye Wayback Machine. (Kiitalia)
- "St. Lucy" from New Advent's Catholic Encyclopedia.
- Representations of Saint Lucy Ilihifadhiwa 3 Aprili 2010 kwenye Wayback Machine.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
