Nenda kwa yaliyomo

Kijerumaniki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lugha za Kijerumaniki)

Lugha za Kijerumaniki ni kikundi cha lugha zenye asili ya Ulaya ya Kaskazini.

Lugha za Kijerumaniki zenye wasemaji wengi ni Kiingereza (milioni 380) na Kijerumani (milioni 120). Lugha nyingine za Kijerumaniki ni lugha za Skandinavia, halafu Kiholanzi na Kiafrikaans wa Afrika Kusini.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzo wa lugha hizi uko gizani. Wataalamu wamejaribu kutambua sifa za lugha asilia kwa kulinganisha lugha mbalimbalimbali zilizo karibukaribu ikiwa habari zao zimejulikana.

Kutokana na makisio hayo Kijerumaniki kilianza Ulaya ya Kaskazini, labda Sweden ya Kusini katika miaka elfu ya kwanza K.K..

Wasemaji wa Kijerumaniki walianza kuhamahama wakati wa Dola la Roma na ndipo habari za kwanza za kihistoria zimepatikana.

Matembezi ya Wajerumaniki yalifika hadi Urusi wa Kusini na Afrika ya Kaskazini.

Lugha za Kijerumaniki katika Ulaya; buluu: Kijerumaniki cha kaskazini; njano: Kijerumaniki cha magharibi tawi la Kifrisia-Kiingereza; kibichi: Kijerumaniki cha magaharibi tawi la Kusini

Lugha za Kijerumaniki hugawanywa katika aina tatu:

a) Kijerumaniki cha Kaskazini: Kiswidi, Kidenmark, Kinorwei, Kiiceland na Kifaroe

b) Kijerumaniki cha Magharibi: Kiingereza, Kijerumani (Kidachi), Kiholanzi, Kiafrikaans, Kijerumani ya Kaskazini, Kifrisia, Kiyiddish (Kiyahudi cha Ulaya)

c) Kijerumaniki cha Mashariki: lugha hizi kama Kivandali au Kigoti zimekufa zote; zinajulikana kama lugha za kihistoria tu