Lugha za Kiberiberi
Aina za Tamazight au lugha za Kiberber katika Afrika ya Mashariki. | |
Kitwareg | Kizayani |
Kirifi | Kishanawa |
Kikabile | Kishawia |
Kishilha | Kiberiberi ya Sahara |
Kiberiberi au Kiamazighi ni jina la kundi la lugha zinazosemwa hasa Moroko na Aljeria lakini pia kati ya wakazi wa jangwa kubwa la Sahara hadi eneo la Sahel. Ni lugha ya Waberiberi wanaoishi kati ya wasemaji wa Kiarabu katika Afrika ya Kaskazini.
Kiberiberi ni kati ya lugha za Kiafrika-Kiasia. Wasemaji wa Kiberiberi watazamiwa kuwa wenyeji asilia wa Afrika ya Kaskazini kabla ya kuja kwa Waroma wa Kale au kwa Waarabu.
Tangu uenezaji wa Kiarabu matumizi ya Kiberiberi kimerudi nyuma polepole. Wakazi wengi wa nchi za Afrika ya Kaskazini ni wa asili ya Kiberber lakini kwa kawaida kupotea kwa lugha humaanisha pia upotevu wa tabia ya kuwa Berber. Leo hii wamebaki wasemaji milioni 10 na wengi wao hutumia lugha yao pamoja na Kiarabu au Kifaransa katika maisha ya kila siku.
Mwandiko
[hariri | hariri chanzo]Kiberiberi kimeandikwa tangu miaka maelfu. Mifano ya kale kabisa imehifadhiwa tangu 200 KK iliyoandikwa kwa mwandiko wa Tifinagh unaoendelea kutumiwa na Watuareg.
Aina ya Tifinagh imekuwa mwandiko rasmi nchini Moroko tangu mwaka 2003 pamoja na Kiarabu na Kilatini.
Tangu mwaka 1000 na uenezaji wa Uislamu lugha imeanza kuandikwa kwa herufi za Kiarabu.
Katika karne ya 20 imeandikwa mara nyingi kwa mwandiko wa Kilatini.
Katika nchi nyingi zilikuwa koloni za Ufaransa mwandiko ni Kilatini hadi leo.