Nenda kwa yaliyomo

Ludwig Draxler

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ludwig Draxler (1896-1972) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa wa Austria.

Draxler alikuwa mzee aliyepambana Vita Kuu ya Kwanza na aliwahi kuwa Katibu wa Fedha wa Austria kutoka 1935-1936. Mwaka 1938 Chama cha Nazi kilimkamata kwa kukataa Austria kuingizwa katika Ujerumani akafungwa katika kambi la maangamizi la Dachau.

Baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Pili, alianzisha tena ofisi yake huko Vienna. Wateja maarufu, kati ya wengine, walikuwa Otto von Habsburg, mwana wa kwanza wa Karl wa Austria, Mfalme wa mwisho wa Austria na wa Hungary. Draxler alikuwa na jukumu muhimu katika "Causa Habsburg" ambayo ilisababisha kurudi kwa Otto von Habsburg kwa Austria kama raia wa kawaida mwaka 1966 baada ya miaka 48 uhamishoni.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ludwig Draxler kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.