Lassana Coulibaly

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lassana Coulibaly

Lassana Coulibaly, (alizaliwa 10 Aprili, 1996) ni mchezaji mzuri wa soka nchini Mali ambaye anacheza kama kiungo wa Klabu ya Ubelgiji Cercle Brugge K.S.V., kwa mkopo kutoka katika klabu ya Angers SCO, na timu ya taifa ya Mali.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Angers[hariri | hariri chanzo]

Coulibaly ni mchezaji wa vijana kutoka Bastia na alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligue 1 mnamo 8 Agosti 2015 dhidi ya Rennes.

Aliingia kama mbadala wa François Kamano katika mechi ya ushindi wa 2-1 nyumbani.Wiki mbili baadaye, alifunga goli lake la kwanza la ligi dhidi ya Guingamp.

Mnamo 10 Julai 2018, Coulibaly alijiunga na Washikaji wa Shirikisho la Soka la Scottish kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka kwa Anger.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Coulibaly aliitwa katika timu ya taifa ya chini ya miaka 20 ya Mali kwa Mashindano ya Toulon ya mwaka 2016, na akachezaa mechi yake ya kwanza kwa kupoteza dhidi ya Jamhuri ya Czech chini ya miaka 20. Alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya taifa ya Mali katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2017 ambao walipata ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya Benin mnamo 4 Septemba 2016.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lassana Coulibaly kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.