Nenda kwa yaliyomo

Lambo la Mwenga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lambo la Mwenga ni lambo liliounda bwawa la kuzalisha umeme nchini Tanzania, linalopatikana katika Mkoa wa Iringa. Uwezo wake uliowekwa ni megawati 4 (5,400 hp). Kiwanda hicho cha nishati kinaendeshwa na mzalishaji huru wa nishati, Rift Valley Energy.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mtambo huo ni sehemu ya mradi wa kusambaza umeme wa Mwenga Hydro na Rural Electrification Mini Grid. Kiwanda hicho kilijengwa ili kusambaza umeme kwenye mashamba ya mchai ya Mufindi na kilijengwa takriban kilomita 50 kutoka kiwandani. Kando ya njia ya usafirishaji kulikuwa na vijiji 17 visivyo na umeme. Rift valley energy iliamua kuunganisha vijiji hivyo na kuvipatia umeme.

Kampuni ilipata msaada kutoka kwa Shirika la Nishati la ACP-EU na Wakala wa Nishati Vijijini Tanzania, na mwaka 2012 ilizindua mtambo wa 4MW Hydro na gridi ndogo. Kufikia mwaka wa 2020, kampuni hiyoi inatoa nishati kwa Kiwanda cha Chai na vilevile kwa vijiji 32 katika wilaya ya Mufindi vinavyohudumia wateja 4800.

Rift Valley Energy inaendesha huduma zake za usambazaji umeme kupitia Mwenga Power Services Ltd.