Kwando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mto wa Kwando (Cuando)
Mto Kwando (kushoto) unaingia Mto Zambezi kwenye mji wa Kazungula (kulia katikati)
Chanzo Nyanda za juu za Bié (Angola)
Mdomo Mto Zambezi kwa mji wa Kazungula (Zambia)
Nchi Angola, Zambia, Namibia, Botswana
Urefu 1,500 km
Kimo cha chanzo 1,700 m takriban
Mkondo ??
Eneo la beseni 96,778 km²

Kwando (au: Cuando; kabla ya mdomo pia Linyanti halafu Chobe) ni mto wa Afrika ya Kusini na tawimto wa Zambezi. Chanzo chake iko nyanda za juu za Bié (Angola) inapoelekea kusini-mashariki. Inakuwa mpaka kati ya Angola na Zambia kwa 140 km halafu inapita Kishoroba cha Caprivi na kuwa mpaka kati ya Namibia na Botswana.

Inaingia katika mabwawa wa Linyanti yenye 1,425 km². Katika sehemu hizi mto huitwa kwa majina Chobe au Liyanti.

Kwa jina la Chobe unaingia katika mto Zambezi kwenye mji wa Kazungula pale ambako nchi nne za Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe zinakutana.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]