Koreshi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Koreshi ni jina la kiume lenye asili ya Kiajemi linakopatikana kwa umbo la "کوروش" (Kurush au Kurosh). Umbo "Koreshi" lililo kawaida katika Kiswahili linatokana na כורש (koresh) umbo la Kiebrania la jina hilo katika taarifa za Biblia.

Kuna maelezo tofauti kuhusu maana asilia ya jina. Inaweza kumaanisha ama "mtawala mshindi mwenye huruma" au "kijana, mtoto".

Linafahamika hasa kutokana na wafalme wa Uajemi ya Kale hasa Koreshi I na Koreshi Mkuu walioanzisha na kupanua milki ya kwanza ya Uajemi.

Hadi leo ni jina la wanaume nchini Uajemi na kwingine kwa maumbo kama: