Nenda kwa yaliyomo

Kokoro (wimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kokoro)
“Kokoro”
“Kokoro” cover
Kava ya Kokoro (wimbo)
Single ya Rich Mavoko akiwa na Diamond Platnumz
Imetolewa 22 Novemba, 2016
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2016
Aina Afro pop, Bongo Flava
Urefu 3:27
Studio WCB
Mtunzi Rich Mavoko
Diamond Platnumz
Mtayarishaji Laizer
Abby Daddy
Mwenendo wa single za Rich Mavoko akiwa na Diamond Platnumz
"Ibaki Story"
(2016)
"Kokoro"
(2016)
"Sheri"
2017

"Kokoro" ni jina la wimbo uliotoka 22 Novemba, 2016 wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Rich Mavoko akishirikiana na Diamond Platnumz. Huu ndio wimbo wa kwanza kushirikiana na Diamond tangu kujiunga na WCB na wa pili kutolewa baada ya wa kwanza Ibaki Story iliyotoka mwezi Juni, 2016.

Wimbo umetayarishwa na watayarishaji wawili tofauti. Awali ulifanywa nusu na Abby Daddy ukaja kumaliziwa na Laizer katika studio za Wasafi Records. Wimbo huu ndio ulioleta mtafaruku baina ya Ali Kiba na mtayarishaji wake Abby Daddy. Kulingana na Abby, Kiba ilionekana kutaka kumdhibiti Abby asitengeneze nyimbo na mtu mwingine yeyote isipokuwa yeye au iwe mwingine lakini si WCB. Kitendo hiki kilimuumiza sana Abby na kutoa ya moyoni.[1]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Majadiliano juu ya mgogoro wa Abby Daddy na Kiba Abby dad ametengeza hits kama #Nagharamia #Chekecha Cheketua na #Aje ambazo zilifanya vizuri sana.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]