Kiti moto
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kitimoto)
Kiti moto ni aina ya chakula maarufu nchini Tanzania kinapoitwa pia "mdudu" au "mbuzi katoliki". Sehemu kuu ya chakula hiki ni nyama ya nguruwe.
Inaaminika kuwa chanzo cha jina hili ni nia ya kutumia neno la siri kwa kuwa Waislamu hawatakiwi kula nguruwe.
Chakula hiki kinapikwa pale mtu anapotoa oda yake na hivyo kukaa kwenye kiti kwa hata zaidi ya saa moja akisubiri kwa hamu, hivyo ni kama kikao kirefu cha mahojiano kinachomtesa mtu kwa kumdai atetee kwa hoja nzito jambo fulani, k.mf. utendaji wake, ambacho pia kinaitwa kitimoto.
Baadhi ya migahawa hutenga sehemu maalum ya kula kitimoto kwa heshima ya wateja ambao ni Waislamu.
Kiti moto ni maarufu sana kwenye sehemu za starehe na pombe.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Mapishi ya kiti moto Ilihifadhiwa 18 Julai 2019 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiti moto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |