Kijiko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kijiko cha chuma
Kijiko (Tanzania)

Kijiko ni kifaa chenye umbo la duara lililobonyea kinachotumika wakati wa kula au mara nyingine kupakulia chakula.

Kimsingi vijiko hutumika kula vyakula rojorojo, kama vile supu, mchemsho na lambalamba, pia vyakula vidogovidogo na vilivyo ungaunga ambavyo haviwezi kuinuliwa kwa uma kama vile wali, sukari na nafaka.

Kwenye uokaji rojo ni laini sana kumimina au kudondosha kutoka kwenye kijiko.

Vijiko hutumika pia katika kupima, kuchanganya na kukoroga vitu mbalimbali kama vile viungo.

Vijiko hutumika pia kukorogea, kwa njia hii kijiko hupitishwa katika mchanganyiko na huzungushwazungushwa katika maduara ili kusaidia mchanganyiko huo uchanganyike kikamilifu.

Vijiko hutumiwa sana katika mapishi na upakuaji wa chakula.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mifano ya vijiko mbalimbali vilivyotumiwa na [[Wamisri wa kale]] inahusisha vilivyotengenezwa kwa pembe za ndovu, mawe na mbao; vingi vilitiwa nakshi kwa alama za kidini.

Vijiko vya Wayunani na Warumi wa kale vilitengenezwa kwa shaba na fedha na mishikio yake ilikuwa imechongoka.

Siku hizi vijiko hutengenezwa kwa metali kama fedha, pia kwa mbao, plastiki na kauri.

Katika Asia ya Kaskazini, vijiko hutumika kama chombo cha msingi kwa ajili ya kula; uma zinatumika kusukuma vyakula kama wali kwenye vijiko pia na matumizi yake ya kawaida kama kukatia au kugawanyishia chakula.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kijiko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.