Kigong'ota
Vigong'ota, gongonola, gogota, vigotagota au ving'ota ni ndege wa nusufamilia Picinae katika familia Picidae. Ni bora kutengea spishi za nusufamilia Picumninae jina “kigogota”. Inawakilishwa katika Afrika na kigogota wa Afrika. Vigong'ota vinatokea misituni na maeneo mengine yenye miti kila mahali pa dunia isipokuwa Madagaska, Australia, New Zealand na kanda za Aktiki na Antaktiki.
Spishi nyingi ni nyeusi mgongoni kwenye madoa na/au mabaka meupe au njano. Spishi nyingine zina rangi ya majani au kahawa. Miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Mkia una manyoya shupavu na umsaidia ndege kutembea wima mashinani kwa miti. Ndege hawa wana domo lenye nguvu ambalo hutumia kugogota miti na kutafuta wadudu katika nyufa za miti. Ulimi wao mrefu wa kunata na wenye nywele uwasaidia kuwatoa wadudu. Zaidi ya wadudu vigong'ota hula matunda na makokwa; spishi nyingine hula hata utomvu wa miti. Dume huchimba tundu katika mti na pengine jike amsaidia. Huyu huyataga mayai 2-6 ndani ya tundu.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Campethera abingoni, Kigong'ota Mkia-njano Golden-tailed Woodpecker)
- Campethera bennettii, Kigong'ota Masharubu-mekundu (Bennett's Woodpecker)
- Campethera cailliautii, Kigong'ota Mgongo-kijani (Green-backed Woodpecker)
- Campethera caroli, Kigong'ota Masikio-kahawia (Brown-eared Woodpecker)
- Campethera maculosa, Kigong'ota Miraba (Little Green Woodpecker)
- Campethera mombassica, Kigong'ota wa Mombasa (Mombasa Woodpecker)
- Campethera nivosa, Kigong'ota Kisogo-chekundu (Buff-spotted Woodpecker)
- Campethera notata, Kigong'ota wa Knysna (Knysna Woodpecker)
- Campethera nubica, Kigong'ota Nubi (Nubian Woodpecker)
- Campethera punctuligera, Kigong'ota Madoa-madogo (Fine-spotted Woodpecker)
- Campethera scriptoricauda, Kigong'ota Vipaku Speckle-throated au Reichenow's Woodpecker)
- Campethera tullbergi, Kigong'ota Miraba au Gongonola (Tullberg's Woodpecker)
- Chloropicus namaquus, Kigong'ota Kidevu-cheusi (Bearded Woodpecker)
- Chloropicus pyrrhogaster, Kigong'ota Tumbo-jekundu (Fire-bellied Woodpecker)
- Chloropicus xantholophus, Kigong'ota Kishungi-njano (Yellow-crested Woodpecker)
- Dendrocopos major, Kigong'ota Madoa-meupe Mkubwa (Great Spotted Woodpecker)
- Dendropicos abyssinicus, Kigong'ota Habeshi (Abyssinian Woodpecker)
- Dendropicos elachus, Kigong'ota Kijivu Mdogo (Little Grey Woodpecker)
- Dendropicos elliotii, Kigong'ota wa Elliot (Elliot's Woodpecker)
- Dendropicos fuscescens, Kigong'ota Mgongo-miraba (Cardinal Woodpecker)
- Dendropicos gabonensis, Kigong'ota wa Gaboni (Gabon Woodpecker)
- Dendropicos goertae, Kigong'ota Kijivu (African Grey Woodpecker)
- Dendropicos griseocephalus, Kigong'ota Zeituni (Olive Woodpecker)
- Dendropicos lugubris, Kigong'ota Huzuni (Melancholy Woodpecker)
- Dendropicos obsoletus, Kigong'ota Mgongo-mwekundu Brown-backed Woodpecker)
- Dendropicos poecilolaemus, Kigong'ota Kidari-madoa (Speckle-breasted Woodpecker)
- Dendropicos spodocephalus, Kigong'ota Kichwa-kijivu (Eastern Grey Woodpecker)
- Dendropicos stierlingi, Kigong'ota-miyombo (Stierling's Woodpecker)
- Dryobates minor, Kigong'ota Madoa-meupe Mdogo (Lesser Spotted Woodpecker)
- Geocolaptes olivaceus, Kigong'ota-ardhi (Ground Woodpecker)
- Picus vaillantii, Kigong'ota Kijani wa Afrika (Levaillant's Woodpecker)
Jenasi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Blythipicus (spishi 2)
- Campephilus (spishi 11)
- Celeus (spishi 11)
- Chrysocolaptes (spishi 8)
- Chrysophlegma (spishi 3)
- Colaptes (spishi 13)
- Dendrocopos (spishi 12)
- Dinopium (spishi 4)
- Dryobates (spishi 5)
- Dryocopus (spishi 7)
- Gecinulus (spishi 2)
- Hemicircus (spishi 2)
- Meiglyptes (spishi 3)
- Melanerpes (spishi 24)
- Micropternus (spishi 1: Rufous Woodpecker)
- Mulleripicus (spishi 3)
- Picoides (spishi 12)
- Piculus (spishi 7)
- Picus (spishi 12)
- Reinwardtipicus (spishi 1: Orange-backed Woodpecker)
- Sapheopipo (spishi 1: Okinawa Woodpecker)
- Sphyrapicus (spishi 4)
- Veniliornis (spishi 14)
- Xiphidiopicus (spishi 1: Cuban Green Woodpecker)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kigong'ota masharubu-mekundu
-
Kigong'ota mgongo-kijani
-
Kigong'ota wa Mombasa
-
Kigong'ota Nubi
-
Kigong'ota madoa-madogo
-
Kigong'ota miraba
-
Kigong'ota kidevu-cheusi
-
Kigong'ota tumbo-jekundu
-
Kigong'ota kishungi-njano
-
Kigong'ota madoa-meupe mkubwa
-
Kigong'ota Habeshi
-
Kigong'ota Mgongo-miraba
-
Kigong'ota kijivu
-
Kigong'ota kijanikijivu
-
Kigong'ota huzuni
-
Kigong'ota kichwa-kijivu
-
Kigong'ota madoa-meupe mdogo
-
Kigong'ota-ardhi
-
Kigong'ota kijani wa Afrika
-
Magellanic woodpecker
-
Blond-crested woodpecker
-
Greater flameback
-
Northern flicker
-
Green-barred woodpecker
-
Himalayan woodpecker
-
Syrian woodpecker
-
Black-rumped flameback
-
Common flameback
-
Andaman woodpecker
-
Black woodpecker
-
Heart-spotted woodpecker
-
Golden-fronted woodpecker
-
Red-bellied woodpecker
-
White-headed woodpecker
-
Downy woodpecker
-
Grey-headed woodpecker
-
Eurasian green woodpecker
-
Red-naped sapsucker
-
Red-breasted sapsucker