Kicheche
Mandhari
Kicheche | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kicheche-nyoka (Poecilogale albinucha)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 4, spishi 6:
|
Vicheche au cheche ni wanyama wa jenasi mbalimbali katika familia Mustelidae. Wanyama hawa ni miongoni mwa wale wanaotoa vundo mbaya kabisa. Wataalamu wengine wanadai kwamba kicheche wa kawaida ananuka vibaya kuliko wanyama wote. Vundo hii inatoka matezi karibu na mkundu kama mnyama akitishwa, na kwa kawaida adui atoroka. Spishi zote zina pua, kidari, tumbo na miguu nyeusi. Zile za Afrika zina milia myeupe na myeusi mgongoni, zile za Amerika zina mgongo kijivu na ile ya Ulaya ina mgongo njano wenye madoa meusi. Vicheche hula wanyama wadogo, ndege na mijusi, wadudu, samaki, amfibia, nyoka na hata matunda na manyasi.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Ictonyx libycus, Kicheche-jangwa (Sahara Striped Polecat)
- Ictonyx striatus, Kicheche wa Kawaida (Striped Polecat or Zorilla)
- Poecilogale albinucha, Kicheche-nyoka (African Striped Weasel)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Galictis cuja, Kicheche Mdogo wa Amerika (Lesser Grison)
- Galictis vittata, Kicheche Mkubwa wa Amerika (Greater Grison)
- Vormela peregusna, Kicheche Madoa (Marbled Polecat)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kicheche-jangwa
-
Kicheche wa kawaida
-
Kicheche mdogo wa Amerika
-
Kicheche mkubwa wa Amerika
-
Kicheche madoa