Kiboriloni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiboriloni ni kata ya Moshi Mjini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania yenye postikodi namba 25113[1].

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,206 [2] walioishi humo. Wananchi wa kata hii wanajishughulisha na biashara ndogondogo kama uuzaji wa mbogamboga na matunda na pia wanajishughulisha na zao la ndizi. Makabila yafuatayo yanapatikana katika kata hiyo: Wachagga, Wapare, na mengineo mengi.

Ndani ya kata hii ya Kiboriloni kuna ikulu ndogo ambayo Rais huwa anaitumia kwa ajili ya mapumziko akiwa na ziara katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Boma Mbuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiboriloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kiboriloni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.