Kazi za wanawake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kazi za wanawake mara nyingi huchukuliwa kama ni kazi zinazowahusu wanawake pekee, na huhusishwa na kazi hizo kutokana na jinsia ya kike katika historia. Mara nyingi huchukuliwa kama kazi isiyolipwa ambayo mama au mke hufanya nyumbani na kwenye familia. [1]

Kazi za wanawake kwa ujumla si za kulipwa au hulipwa kidogo ukifananisha na "kazi za wanaume" na haithaminiwi sana kama hizo. [2] Kazi nyingi za wanawake hazijajumuishwa katika takwimu rasmi za kazi za nyumbani, na kusababisha kazi nyingi ambazo wanawake hufanya kwa kawaida zisionekane. [3] Kwa mfano, katika sehemu kubwa ya karne ya 20, wanawake wanaofanya kazi katika shamba la familia, bila kujali ni kazi ngapi walizofanya, walihesabiwa katika sensa ya Marekani kama awana ajira, wakati wanaume wanaofanya kazi sawa au hata kidogo walihesabiwa kama wanaofanya kazi kama wakulima.

Aina za kazi[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina kadhaa za kazi zinazoonwa kuwa za wanawake; zinahusisha kutunza watoto, kazi za nyumbani, na kazi kama vile uuguzi ambazo zimetawaliwa na wanawake katika miongo ya hivi karibuni.

Huduma ya watoto[hariri | hariri chanzo]

Neno "kazi za wanawake" unaweza kumaanisha daraka la kuwatunza watoto kama linavyofafanuliwa na asili kwa kuwa ni wanawake tu wanaoweza kufanya kazi hizo: ujauzito, kuzaa, na kunyonyesha . Inaweza pia kurejelea fani zinazohusisha kazi hizi: mkunga na nesi . "Kazi ya wanawake" inaweza pia kurejelea majukumu kama kulea watoto, haswa ndani ya nyumba: kubadilisha nepi na usafi unaohusiana, kuwazoeza kutumia choo, kuoga, kuvaa, kuwalisha, kuwachunguza, na kuwafundisha jinsi ya kujitunza.

Wanawake wanaofanya kazi katika muda wa kupumzika

Viwanda vinavyotawaliwa na wanawake[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya wanawake pia inaweza kurejelea fani zinazojumuisha malezi ya watoto kama vile mlezi, yaya, mfanyakazi wa kulelea watoto mchana pia nyadhifa za kitaaluma kama vile ualimu (hasa kufundisha watoto) na wauuguzi .

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Borck (September 2019). 'A woman's work is never done': women's working history in Europe (en-GB). Europeana (CC BY-SA). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-09-27. Iliwekwa mnamo 2019-09-27.
  2. Seager, Joni (2018). The Women's Atlas. Oxford: Myriad Editions. pp. 123, 126. 
  3. Seager, Joni (2018). The Women's Atlas. Oxford: Myriad Editions. pp. 125.