Utunzi wa mtoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utunzi wa mtoto, huduma ya mtoto, au kushighulikia mtoto ni kitendo cha kutunza na kulea mtoto wa umri wa miaka 0-16.

Huduma ya watoto ni pana na kufunikia mada pana ambayo ni wigo wa mazingira, shughuli na mikusanyiko ya kijamii na kiutamaduni, na taasisi.

Majukumu ya Kulea Mtoto[hariri | hariri chanzo]

Child Care

Ni jadi katika jamii za magharibi kwa watoto kutunzwa na mzazi mmoja au wote wawili. Katika familia ambapo watoto wanaishi na mmoja au wawili wa wazazi wao, jukumu la kulea watoto pia linaweza kuchukuliwa na ndugu na marafiki. Ikitokea kutokuwepo mmoja au wazazi wote wawili au jamaa tayari kuwatunza mtoto vituo vya yatima ni njia nyingine ya kutoa huduma kwa watoto, makazi, na shule.

Aina kuu tatu za huduma kwa watoto za nyingi za familia za Marekani zinazofanya ni huduma za nyumbani, huduma za familia, na vituo vya huduma ya watoto. Familia nyingi za Marekani hufanya kazi mara mbili, na hii ina maana kuwa mara nyingi kazi kulea watoto hupewa wanaotunza watoto au yaya siku nzima au masaa machhe.

Huduma nyumbani zinazotolewa kwa kawaida ni yaya, au marafiki na familia. Mtoto anaangaliwa akiwa nyumbani au kituo cha kutunza watoto, kupunguza mfiduo ya watoto na magonjwa. Kutegemea idadi ya watoto walio nyumbani, watoto wanaochukulia fursa hii ya huduma za nyumbani vizuri kufurahia huduma yhufurahia mwingiliano mkubwa na anayemtunza na kuunda urafiki wa kudumu. Hakuna leseni inayohitajika kama njia ya kuangalia utunzi wa nyumbani, kwa hivyo ni jukumu la wazazi kuchagua watunzi watoto vwanaofaa. Huduma za yaya huwa na walezi waliothibitishwa na gharama za huduma za nyumbani huwa juu ingawa familia inayo watoto wengi wanaweza wanapendelea chaguo hili.

Huduma za familia zinazotolewa katika nyumba ya mlezi mtoto ambayo mazingira yake ni sawa na nyumbani kwa mtoto. Mahitaji ya leseni hutafautiana,kwa hivyo mzazi anatakiwa kufanya mahojiano kwa makini na kutembelea nyumba hizo, vilevile kukamilisha kukagua leseni ya mwenye kupatiana huduma hizi za mtoto. Malalamiko yoyote dhidi ya mlezi mtoto itawekwa kwenye rekodi kwa ajili ya umma. Huduma ya familia kwa ujumla ni nafuu zaidi katika chaguo za kulea watoto, na huwa na masaa yanayoweza kubadilika katika utunzaji wa mtoto. Huduma ya familia kwa ujumla ina uwiano wa watoto wadogo katika huduma, na kuruhusu mwingiliano zaidi kati ya mtoto na mlezi kuliko vile iko katika kituo cha kibiashara cha huduma za watoto.

Vituo vya kibiasharavya huduma ya watoto yaliyopangwa ya kazi, na kutoa mfumo uliopangwa za huduma kwa watoto. Wazazi wanaweza kuchagua kutoka kituo cha biashara cha huduma ya mtoto karibu na kazi zao, na baadhi ya makampuni hutoa huduma katika vituo vyao. Watoto waliochangamka huweza kustawi katika shughuli za elimu zinazotolewa na vituo bora za huduma. Madarasa ni kawaida huwa kubwa katika aina hii ya huduma.Uiwano wa watoto nawalezi wazima hutofautiana kulingana na mahitaji ya leseni.

Bila kujali aina ya huduma ya iliyochaguliwa, mtoa huduma bora anapaswa kumpatia mtoto mwanga, angavu safi na maeneo ya kucheza na vile vile mahala tofauti pa kula na kulala v.

Nchi za magharibi pia huwa na elimu ya lazima wakati ambapo wengi wa watoto huwashuleni kuanzia miaka tano au umri wa miaka sita. Shule itatenda kazi yake katika parentis loco amabayo maana yake ni katika lieu ya usimamizi wa mzazi".

Athari katika maendeleo ya mtoto[hariri | hariri chanzo]

Kwa wengi, matumizi ya kulipa kulea watoto ni suala la uchaguzi kwa hoja pande zote kuhusu kama hii ni faida au madhara kwa watoto.

Miaka michache ya kwanza ya maisha ya mtoto ni muhimu kuunda msingi mzuri wa elimu, maadili, kujiamini na nidhamu na kushirikiana na jamii. Ubora wa mbinu hii, ujuzi na sifa ya kazi inavyoonekana katika masomo mengi ni kuwa kuboresha nafasi ya watoto kufikia ujuzi wao. Hata hivyo, chaguo la malezi ya watoto yanaweza kuwa ngumu mno, hata mateso kwa wazazi. Wanasayansi wa kijamii hivi karibuni walianza kuunda hadithi maarufu kamamashujaa wa mijini ili kufichua baadhi ya tata za kijamii na kisaikolojia vipengele katika maamuzi, ambavyo mara nyingi huhusika kwa wazazi wa kiwango cha kati [1] Hapa pia kuna uwezo wa kuona ushawishi wa njia ya awali ya vipengele vyakuhadithia kama vilehadithi za Grimm ambapo watoto hujifunza kuhusu hatari ya kuruhusu watu wasiojua kuingia nyumbani.

Kwa mfano, utafiti wa karibuni katika Australia [2] ulihitimisha kuwa vituo vinavyoendeshwa na kampuni ni huduma za kiwango ya c chini ikilinganishwa na vituo vya kibinafsi na vya kijamii.

Katika sehemu nyingi, serikali inawajibika kwa ufuatiliaji wa ubora wa huduma. Kwa mfano, katika Scotland Her Majesty's mkaguzi wa Elimu ana wajibu wa kuboresha huduma na elimu kwa watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka kumi na minane. Hii hutekelezwa kwa ukaguzi unaofanywa na HMIE au na wanachama wengine wa timu ya ukaguzi na tathmini. Taarifa za ukaguzi huwa mrejesho kutoka kwa wafanyakazi pamoja na wazazi vilevile akina inspekta, wakiwa na lengo la kutoa taarifa kwa wazazi na walezi kuwasaidia kuamua kama kituo cha huduma za mtoto kinahuduma bora. viwango. [3]

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Robin Croft (2006), Folklore, familia na hofu: kuelewa matumizi ya maamuzi kwa njia ya mdomo na mapokeo, Journal of Marketing Management, 22:9 / 10, pp1053-1076, ISSN 0267-257X
  2. 2006, Rush, Taasisi ya Australia http://www.tai.org.au/documents/downloads/DP84.pdf Archived 23 Februari 2011 at the Wayback Machine.
  3. "Childproof Your Home!". Published by VeryTogether.com Published 3 Aprili 2009. Iliwekwa mnamo 2009-05-20. {{cite web}}: External link in |publisher= (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]