Katulino na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Katulino na wenzake Adauti, Felisi, Florenti, Fortunansiani, Januari, Julia, Setimini na Yusta (walifariki Karthago, leo nchini Tunisia, 15 Julai 303) ni kati ya Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian[1].

Katulino alikuwa shemasi na Augustino wa Hippo alitoa hotuba moja juu yake.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 15 Julai[2][3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.