Kasulu
Kasulu ni mji wa Mkoa wa Kigoma magharibi mwa Tanzania yenye msimbo wa posta 47301.
Inatawaliwa na halmashauri yake, hivyo huwa na hadhi ya wilaya tangu enzi za ukoloni. Awali mji wa Kasulu ulitawaliwa pamoja na wilaya ya Kasulu Vijijini kama wilaya moja ila tangu 2012 ni wilaya mbili za pekee.
Eneo la manispaa ni km² 911.[1]
Wakati wa sensa ya mwaka 2012 ilikuwa na wakazi 208.244. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 238,321 [2].
Kasulu iko karibu na mpaka wa Burundi. Baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi wakimbizi wengi walikimbia Tanzania na makambi makubwa yalijengwa karibu na mji wa Kasulu. Makambi haya ni Muyovosi, Mtabila I and Mtabila II. Mnamo mwaka 2000 idadi ya wakimbizi ilifikia 90,000.
Makambi yaliongeza biashara ya eneo lakini yalileta pia matatatizo kama kupanda kwa bei na upungufu wa usalama kwa sababu ujambazi ulizidi.
Kasulu ni makao makuu ya Dayosisi ya Magharibi ya Kanisa Anglikana Tanzania. Kanisa kuu ni St Andrew's Cathedral. Askofu wake alikuwa Gerard Mpango.
Taasisi muhimu ni chuo cha ualimu cha Kasulu Teacher Training College.
Kasulu kuna shule mbalimbali pamoja na Kasulu Bible College ya Kanisa la Kianglikana.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya shirika ya Kiholanzi ya kusaidia watoto wa Kasulu Ilihifadhiwa 6 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya mradi wa mtandao mjini Kasulu Ilihifadhiwa 13 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Ukurasa wa dayosisi ya Kanisa Anglikana Ilihifadhiwa 19 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Taarifa ya mgeni kwenye ibada ya St Andrews
- Tovuti ya Chuo cha Biblia Kasulu Ilihifadhiwa 4 Agosti 2018 kwenye Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Kasulu Mjini - Mkoa wa Kigoma - Tanzania | ||
---|---|---|
Heru Juu | Kasulu Mjini | Kigondo | Kimobwa | Kumsenga | Kumnyika | Msambara | Muganza | Muhunga | Murubona | Murufiti | Murusi | Mwilamvya | Nyansha | Nyumbigwa | Ruhita |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kigoma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kasulu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |