Domitian
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kaisari Domitiano)
Titus Flavius Domitianus (24 Oktoba 51 – 18 Septemba 96) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia 14 Septemba, 81 hadi kifo chake. Alimfuata kaka yake Titus.
Domitiano aliimarisha utaratibu wa Dola. Alijitahidi kutafuta maafisa wenye uwezo nje ya familia ya wakubwa wa Senati hivyo alikuta upinzani aliokandamiza vikali.
Alijitahidi kuimarisha pia dini ya Kiroma. Waandishi Wakristo kama Eusebi waliandika karne mbili baadaye kwamba alitesa Wayahudi na Wakristo waliokataa kuabudu miungu ya Roma lakini wataalamu wa siku hizi hawawezi kuthibitisha habari hiyo[1].
Vitabu vya Ufunuo wa Yohane pamoja na waraka wa kwanza wa Klementi viliandikwa wakati ule.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.biblicalarchaeology.org/daily/biblical-topics/post-biblical-period/domitian-persecution-of-christians/ Alternative Facts: Domitian’s Persecution of Christians, tovuti ya biblicalarchaeology.org, iliangaliwa Oktoba 2022
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Roma bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Domitian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |