Justice Tweneboaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Justice Tweneboaa
Amezaliwa 28 Oktoba 2001
Ghana
Nchi Ghana
Kazi yake mwanasoka

Justice Tweneboaa (alizaliwa 28 Oktoba 2001) ni mwanasoka wa Ghana ambaye anacheza kama beki wa Ampem Darkoaa ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya Ghana.[1][2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Tweneboaa alianza uchezaji wake katika timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Ghana, Amem Darkoa. Mnamo 2020, kabla ya msimu wa 2020-21, aliteuliwa kama nahodha wa timu.

Tweneboaa aliwahi kuwa nahodha wa Ghana katika timu za walio chini ya miaka 17 ,miaka 20 na ngazi ya juu. Aliiwakilisha Ghana kwenye Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake U-17 2018, ambapo walipoteza thidi ya Mexico kwenye hatua ya robo finali. Alikuwa mmoja wa wale wawili waliokosa penalti zao. Katika Kombe hilo la Dunia alicheza pamoja na wachezaji kama Mukarama Abdulai na Nina Norshie .[3]

Mnamo Juni 2020, aliitwa kwenye timu kama mmoja wa wachezaji wakuu kwa mechi zao za kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA U-20 2020 na mechi za kirafiki dhidi ya Moroko kati ya Agosti na Oktoba 2020.[4][5]

Mnamo Machi 2018, aliitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya kitaifa kabla ya mechi ya kirafiki dhidi ya Japan walifungwa 7-1.Tweneboaa alikijumuishwa katika kikosi cha Aisha Buhari Cup na kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2022 dhidi ya Nigeria.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Amoh, Rosalind K. (13 September 2021). Black Queens in Lagos for Aisha Buhari Tournament.
  2. Black Queens coach calls 38 players for camping (en). Ghana Football Association (5 July 2021).
  3. Black Maidens XI to face Uruguay in U17 WC opener (en). Ghana Football Association (13 November 2018).
  4. Ahmadu, Samuel (19 November 2020). Basigi names Ghana U20 women's squad for Morocco test. Goal.com.
  5. GFA Communications (14 August 2020). Thirty-one Black Princesses players to resume camping on Friday. Ghana Football Association.
  6. Teye, Prince Narkortu (13 July 2021). Awcon Qualifier: Former Germany U19 striker Beckmann gets Ghana call-up for Nigeria showdown. Goal.com.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Justice Tweneboaa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.