Junior Braithwaite
Franklin Delano Alexander Braithwaite, anafahamika zaidi kwa jina la Junior Braithwaite, (4 Aprili 1949 – 2 Juni 1999) alikuwa mwanamuziki wa reggae kutoka mjini Kingston huko nchini Jamaika. Yeye mwanachama mdogo zaidi kutoka katika kundi la The Wailing Wailers. The Wailing Wailers lilikuwa kundi la sauti ambalo Bob Marley na Bunny Wailer walilianzisha mnamo 1963, pamoja wakiwa na Braithwaite, wakati muziki wa ska ulikuwa maarufu nchini Jamaika.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Braithwaite alikuwa na The Wailers kwa takriban miezi nane na alipata kuimba akiwa kama kiongozi katika nyimbo kama vile "Habits", "Straight and Narrow Way", "Don't Ever Leave Me", na "It Hurts To Be Alone". Alikuwa na sauti bomba sana kwenye The Wailers, kulingana na maelezo ya Coxsone Dodd wa Studio One, ambaye yeye ndiye aliyegundua kipaji cha bendi hiyo. Bob Marley baadaye alieleza ya kwamba, "Junior alikuwa akiimba sauti ya juu. Ambapo siku hizi nimeanza kutambua ya kwamba anaimba kama mmoja kati ya kina Jackson Five. Alipoondoka imetubidi tutafute sauti ambayo ni Bunny, Peter na mimi tungeweza kumudu".
Braithwaite aliuawa mnamo tar. 2 Juni katika mwaka wa 1999 huko nyumbani kwa mwanamuziki mwenzake mjini Kingston, huku akiwaacha Bunny Wailer na Beverley Kelso wakiwa kama wanachama pekee halisi wa Wailers waliobakia.