Jumanne Rajabu Mtambalike
Jumanne Rajabu Mtambalike (aliyezaliwa tar.) ni Mtanzania mwenye asili kutokea mkoa wa Morogoro, Tanzania lakini alikulia katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Familia
[hariri | hariri chanzo]Jumanne ni mtoto wa nne kati ya watoto sita waliozaliwa katika familia yao. Jumanne aliishi katika utoto wake sana huko Grezani Magharibi, Kariakoo.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Jumanne alihitimu shahada ya Computer Science and Electronics kutoka Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mara baada ya kumaliza chuo kikuu, Jumanne alirudi nchini Tanzania. Alipofika nchini alienda Dodoma pamoja na rafiki yake wa karibu sana kuanzisha kampuni inayohusiana na masuala ya teknolojia. Kampuni hii iliweza kufanya kazi kwa muda wa mieze 18 kabla ya kufungiwa na Bodi ya Mapato, TRA.
Mnamo Disemba mwaka 2012, alijiunga na Tanzania Ports Authority. Alifanya kazi hapo kwa miezi miwili kabla ya kuhamia Bodi ya Sayansi na Teknolojia Tanzania. Katika bodi hii alifanya kazi kwa miaka mitatu kuanzia Februari kama Meneja wa kwanza wa kitivo cha ubunifu cha Buni.
Mapema kati ya mwezi Mei na Agosti mwaka 2015 alifanya kazi katika kazi mradi ya World Bank ReFAB Dar.
Mwezi uliofuata aliweza kufanya kazi na Energy Safari, Hivos-International Institute for Environment Development mpaka Disemba mwaka 2015.
Pia aliweza kufanya kazi na Universal Communication Service Access FUnd kwa miezi mitatu kuanzia Februari mwaka 2016. [1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jumanne Rajabu Mtambalike kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |