Nenda kwa yaliyomo

Juan Cuadrado

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cuadrado katika kombe la dunia la 2018 dhidi ya Uingereza wakitolewa kwa mikwaju ya Penati..
Cuadrado akiwa na Juventus FC.

Juan Guillermo Cuadrado (alizaliwa 26 Mei, 1988) ni mchezaji wa soka wa Colombia ambaye anacheza kama winga kwa klabu ya Italia Juventus FC na timu ya taifa ya Colombia.

Yeye anajulikana kwa mtindo wake wa kucheza, ikiwa ni pamoja na kupiga pasi sahihi, pamoja na ujuzi wake wa kukimbiza mpira.

Cuadrado alianza kucheza kama kiungo wa kati na kiungo mkabaji, kabla ya kuhamishwa kwenye nafasi nyingine ambazo sasa anazicheza, mara nyingi hufanya kazi kama winga wa upande wa kulia, katikati ya kushambulia, au mrengo wa nyuma.

Alianza kazi yake huko Independiente Medellín, Cuadrado alihamia Italia mwaka 2009 kujiunga na Udinese. Alitumikia kidogo katika klabu hiyo, alikopwa na Lecce kwa msimu wa 2011-12,Cuadrado alionekana kuwa mchezaji mzuri sana maonyesho yake yalimfanya ahamie Fiorentina. Mnamo Februari 2015, alisainiwa na klabu ya Chelsea. lakini baada ya kucheza kidogo, alikopwa na Juventus, ambapo alishinda Serie A na Coppa Italia.

Cuadrado yupo katika kikosi vya Colombia ambapo aliisaidia nchi yake kufikia robo fainali kwenye mashindano mawili ya Copa América na Kombe la Dunia la FIFA ya 2014 na kombe la dunia la FIFA la 2018.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juan Cuadrado kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.