Nenda kwa yaliyomo

Jeff Bezos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Jeff Bezos
Jeff Bezos
Kazi yakemjasiriamali wa teknolojia, mwekezaji, na mfadhili wa Marekani



Jeffrey Preston Bezos ni mjasiriamali wa teknolojia, mwekezaji, na mfadhili wa Marekani. Yeye ndiye mwanzilishi, mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji, na rais wa kampuni ya Amazon.com, Inc.

Bezos alizaliwa huko Albuquerque, New Mexico, na alikulia Houston, Texas. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Princeton mnamo mwaka 1986 na alipata digrii yake ya uhandisi wa umeme na sayansi ya kompyuta. Alifanya kazi huko Wall Street katika nyanja mbali mbali kutoka mwaka 1986 hadi mwaka 1994. Alianzisha kampuni yake ya Amazon mwishoni mwa mwaka 1994 karibu na barabara kuu ya kutoka New York City kwenda Seattle. Kampuni hiyo ilianza kama duka la vitabu vya mtandaoni na hadi sasa imepanua bidhaa na huduma nyinɡine za e-commerce, pamoja na utayarishaji wa video na sauti,na akili bandia itumikayo kwenye kompyuta na biashara za mtandaoni. Kwa sasa ni kampuni kubwa zaidi ulimwenguni ya uuzaji wa bidhaa mtandaoni, kwa sasa ndio kampuni kubwa zaidi kwa mapato ya mtandaoni, na pia Jeffrey Preston Bezos ndio mtoaji mkubwa zaidi wa misaada minɡi ulimwenɡuni na huduma za biashara za mitandaoni kupitia mkono wake yeye kwa kuanzanzisha Huduma ya Wavuti ya Amazon.

Bezos aliongezea masilahi yake ya kibiashara wakati alipoanzisha utenɡenezaji wa kampuni wa anɡa doɡo na huduma za anga ndogo ya Bluebin mnamo mwaka 2000. Ndege ya uchunguzi ya kwanza ya Blue ilifanikiwa kufika kwenye space au anɡa la kati mnamo mwaka 2015, na kampuni iyo ina mipango ya kuanza biashara ndogo ya kusafiri au kwenda kwenye space au anɡa la kati ya mwaka wa 2019, kwa hiyo watu wanaweza kusafiri kwa kutumia kampuni yake ya ndeɡe. Alinunua kampuni ya gazeti kuu la kila siku la Marekani The Washington Post mnamo mwaka 2013 kwa dola za kimarekani milioni 250 fedha tasirim, na anasimamia uwekezaji wake mwingine wa biashara kupitia mfuko wake uitwao, Bezos Expeditions.

Mnamo 27 Julai 2017, Bezos alikuwa tajiri wa kwanza kwa muda zaidi ulimwenguni wakati utajiri wake ulikadiriwa kuongezeka zaidi ya dola bilioni 90 za kimarekani. Utajiri wake ulizidi dola bilioni 100 kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 24, 2017, na aliteuliwa rasmi kuwa mtu tajiri zaidi ulimwenguni na Forbes mnamo 6 Machi 2018, na mapato ya jumla ya dola bilioni 112 za Kimarekani. Meneja wa mabilionea wa kwanza kwenye faharisi ya utajiri wa Forbes, alipewa jina la "mtu tajiri zaidi katika historia ya sasa" baada ya kuvuka wavu wake kwa onɡezeko la dola bilioni 150 za kimarekani mnamo Julai 2018. Mnamo Septemba 2018, Forbes alimtanɡaza Bezos kama "tajiri mkubwa kuliko mtu yeyote kwenye sayari hii" kwani aliongeza dola bilioni 1.8 kwa thamani yake katika soko la Amazon kwa kifupi ilifika trilioni 1za kimarekani.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jeff Bezos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.