Nenda kwa yaliyomo

Japhet N'Doram

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Japhet N'Doram
Maelezo binafsi
Jina kamili Japhet N'Doram
Tarehe ya kuzaliwa 27 Februari 1966
Mahala pa kuzaliwa    Ndjamena, Chad
Urefu 1.82m
Nafasi anayochezea Mshambulizi
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Amestaafu
Klabu za vijana
Tourbillon FC N'Djamena
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
1989-1990
1990-1997
1997-1998
Tonnerre Yaoundé
Nantes
Monaco
Timu ya taifa
1989-1998 Chad

* Magoli alioshinda

Japhet N'Doram (alizaliwa Ndjamena, 27 Februari, 1966, ni mwanakandanda wa zamani aliyecheza kama mshambuliaji. Alibandikwa jina la "The Wizard" wakati wake wa kucheza kandanda.

Hapo mwanzoni alicheza katika timu ya mtaa ya Tourbillon FC N'Djamena. Ujuzi wake ukamfanya ahamishwe hadi klabu ya Tonnerre Yaoundé (Kamerun), mojawapo ya klabu kubwa katika bara la Afrika. Ujuzi wake wa kufunga mabao mengi katika timu ya Tonnerre Yaoundé katika Ligi Kuu ya Kamerun ya Kandanda ulifanya watafutaji wa talanta kutoka klabu za Uropa waje kumwona. Muda mfupi baadaye akapata uhamisho kuenda mojawapo ya klabu za Ufaransa.

Baadaye, alicheza katika klabu ya FC Nantes nchini Ufaransa. Akiwa huko alifunga mabao mengi sana na muhimu. Hii ilimfanya kupendwa sana Ufaransa na akawa shujaa wa mashabiki wa FC Nantes. Mabao yake muhimu ni kama bao la 2000 la klabu yake katika ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1 na pia bao la ushindi katika mechi dhidi ya Juventus katika shindano la Ligi Kuu ya Mabingwa. Nantes ilishinda mechi hiyo 3-2. Yeye alishinda medali ya ubingwa ya Ufaransa akiwa katika klabu hiyo ya Nantes katika mwaka wa 1995.

Aliendelea kucheza katika klabu ya AS Monaco lakini akastaafu kama mchezaji katika mwaka wa 1998 kufuatia jeraha lililomsumbua baada la kulipata katika mechi dhidi ya Nantes.

Wasifu wake wa Uchezaji

[hariri | hariri chanzo]
Msimu Klabu Mechi Mabao
1985-86 Tourbillon FC N'Djamena
1989-90 Tonnerre Yaoundé 32 18
1990-91 Nantes 19 5
1991-92 Nantes 25 5
1992-93 Nantes 31 10
1993-94 Nantes 26 8
1994-95 Nantes 32 12
1995-96 Nantes 24 15
1996-97 Nantes 35 21
1997-98 AS Monaco 13 1

Wasifu wa kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Alicheza katika mechi 36 katika timu ya taifa ya Chad na akafunga mabao 13 katika timu hiyo.

Wasifu kama Kocha

[hariri | hariri chanzo]

Alijiunga na wafanyikazi wa timu ya Monaco kama skauti wa wachezaji wenye talanta. Alijiunga na timu ya FC Nantes tena mnamo 28 Juni,2005 akichukua nafasi ya Robert Budzynski kama mkurugenzi wa michezo.

  1. (Kiingereza) Playerhistory.com Profile
  2. [1]
  3. (Kifaransa) Detailed discussion of his career
  4. (Kifaransa) Interview with N'Doram